Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 24, 2024 Local time: 22:37

Kiongozi wa zamani wa walio wengi Baraza la Seneti Reid afariki akiwa na miaka 82


FILE - kiongozi wa zamani wa walio wengi katika Baraza la Seneti Harry Reid akitoa mhadhara Chuo Kikuu cha Nevada, Reno, Aprili 3, 2018. (AP Photo/Scott Sonner)
FILE - kiongozi wa zamani wa walio wengi katika Baraza la Seneti Harry Reid akitoa mhadhara Chuo Kikuu cha Nevada, Reno, Aprili 3, 2018. (AP Photo/Scott Sonner)

Harry Reid, kiongozi wa zamani wa walio wengi katika Baraza la Seneti na mbunge wa Nevada aliyehudumu kwa muda mrefu katika Bunge, amefariki nyumbani kwake Henderson, Nevada. Alikuwa na umri wa miaka 82.

Reid alifariki kwa amani Jumanne akiwa amezungukwa na marafiki nyumbani kwake katika kitongoji cha Henderson, “kufuatia miaka minne kwa ushujaa alipambana na saratani ya kongosho kwa mujibu wa wanafamilia na taarifa kutoka kwa Landra Reid, mke wake aliyeishi naye kwa miaka 62.

“Harry alikuwa mtu mwenye kuijali familia na rafiki mkweli sana,” amesema mkewe. “Tunashukuru sana faraja zinazotufikia kutoka kwa wengi kwa miaka michache hii iliyopita. Tunawashuru hasa madaktari na wauguzi waliokuwa wakimhudumia. Naomba mjue kuwa hilo lilikuwa ni jambo kubwa kwake,” Landra Reid alisema.

Mipango ya mazishi itatangazwa katika sku chache zijazo, alisema.

Harry Mason Reid, bondia wa zamani aliyegeuka kuwa wakili alikuwa anatambulika kama mmoja wa watu waliokuwa na msimamo thabiti katika kufikia makubaliano ndani ya Bunge, Mdemokrat mconservative katika bunge lililokuwa limegawanyika aliyefungamana na wabunge wa vyama vyote kwa kuwaeleza ukweli na kauli mbiu yake ilikuwa : “Bora kucheza ngoma badala ya kupigana, lakini najua namna ya kupigana.”

FILE - Seneta Harry Reid
FILE - Seneta Harry Reid

Kwa zaidi ya miaka 34 ya kazi yake hiyo mjini Washington, Reid alijitahidi bila ya kujitangaza kupambana na kulifanya Baraza la Seneti liwe chini ya udhibiti wa chama chake katika kipindi cha marais wawili, Mrepublikan George W. Bush na Mdemokrat Barack Obama -- wakati wa kudorora kwa uchumi na Warepublikan walipochukua Baraza la Wawakilishi baada ya uchaguzi wa 2010.

“Harry aliposema atafanya kitu fulani, alikifanya.” Rais Joe Biden amesema katika taarifa yake baada ya kifo cha mwenzake aliyeshirikiana naye kwa muda mrefu katika Baraza la Seneti. “Iwapo atakupa ahadi, unaweza kuitegemea. Hivyo ndivyo alivyotekeleza mambo kwa ajili ya maslahi ya nchi kwa miongo kadhaa.”

Rais Joe Biden
Rais Joe Biden

Reid alistaafu mwaka 2016 baada ya ajali kumuacha akiwa haoni jicho moja, na kueleza mwezi May 2018 kuwa alikuwa amegundulika ana saratani ya kongosho na anaendelea na matibabu.

Chini ya wiki mbili zilizopita, maafisa na mmoja wa watoto wake, Rory Reid, walihudhuria kubadilishwa jina kwa uwanja wa wenye harakati nyingi wa Las Vegas kuitwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Harry Reid. Rory Reid ni mwenyekiti wa zamani wa Tume ya Clark Kaunti na mgombea wa nafasi ya udiwani kwa tiketi ya Demokratik Nevada.

Wote wawili Harry na Landra Reid hawakuhudhuria tafrija ya Disemba 14 iliyofanyika katika eneo ambalo lilikuwa linajulikana tangu mwaka 1948 kama Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa McCarran, ulioitwa kwa jina la seneta wa zamani wa Marekani kutoka Nevada, Pat McCarran.

Reid alikuwa anajulikana Washington kwa mbinu zake za kushitukiza, akitambulika kwa tabia isiyo ya kawaida ya kukata simu bila ya kuaga.

FILE - Rais Barack Obama, kushoto, and Kiongozi wa Seneti wa zamani wa Walio Wengi Harry Reid Aug. 24, 2015, in Las Vegas.
FILE - Rais Barack Obama, kushoto, and Kiongozi wa Seneti wa zamani wa Walio Wengi Harry Reid Aug. 24, 2015, in Las Vegas.

“Hata pale nilipokuwa rais, alikata simu yangu,” Obama amesema katika salamu zake za kumuenzi Reid kwa njia ya video 2019.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AP

XS
SM
MD
LG