Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 30, 2024 Local time: 21:28

Waziri mkuu wa Somalia azungumza na Afisa wa serikali ya Marekani kuhusu mzozo wa kisiasa wa Somalia


Waziri mkuu wa Somalia Mohamed Hussein Roble akizungumza bungeni, Mogadishu.
Waziri mkuu wa Somalia Mohamed Hussein Roble akizungumza bungeni, Mogadishu.

Waziri mkuu wa Somalia Mohamed Hussein Roble amezungumza kwa njia ya simu na afisa mwandamizi wa Marekani kuhusu hali ya kisiasa  inayojiri Somalia, msemaji wa serikali amesema Jumatano, wakati mivutano ikiendelea kati ya Roble na Rais Mohammed Abdullahi Mohammed maarufu kama Farmajo.

Vikosi vinavyomuunga mkono waziri mkuu Jumanne vilipiga kambi karibu ya ikulu ya rais, na hivyo kuzusha hali ya taharuki katika mji mkuu Mogadishu.

Msemaji wa serikali ya Somalia, Mohamed Ibrahim Moalimu na mshauri mkuu wa Roble, ameandika kwenye Twitter kuwa waziri mkuu alizungumza na Molly Phee, waziri mdogo wa mambo ya nje wa Marekani anayehusika na masuala ya Afrika, na walizungumza kuhusu hali ya kisiasa nchini Somalia, usalama na uchaguzi.

Jumatatu, rais Mohamed alimsimamisha kazi waziri mkuu kwa tuhuma za ufisadi, hatua ambayo waziri mkuu ameikemea kuwa ni jaribio la mapinduzi.

XS
SM
MD
LG