Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 15, 2024 Local time: 10:10

Maafisa wa afya Marekani wapunguza muda wa kujitenga kwa wasio na dalili


Picha ya nembo ya idara ya kudhibiti na kuzuia magonjwa Marekani CDC .
Picha ya nembo ya idara ya kudhibiti na kuzuia magonjwa Marekani CDC .

Maafisa wa afya nchini  Marekani walifupisha muda uliopendekezwa wa kujitenga kwa Wamarekani wasio na dalili za  COVID-19 hadi siku tano kutoka  mwongozo wa awali wa siku 10.

Maafisa wa afya nchini Marekani siku ya Jumatatu walifupisha muda uliopendekezwa wa kujitenga kwa Wamarekani wasio na dalili za COVID-19 hadi siku tano kutoka mwongozo wa awali wa siku 10.

Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa-CDC pia vilisema watu ambao wamepimwa na kukutwa na virusi baada ya kujitenga wanapaswa kufuata siku tano za kuvaa barakoa wanapokuwa karibu na wengine.

Omicron inachukua asilimia 73 ya maambukizi ya corona kote nchini Marekani, CDC ilisema wiki iliyopita.

Maambukizi yanaongezeka kati ya idadi ya watu waliopewa chanjo kamili, pamoja na wale ambao wamepewa chanjo ya tatu ya nyongeza. Hata hivyo, Omicron inaonekana kusababisha dalili zisizo kali zaidi kwa watu hao, ambao baadhi yao hawana dalili zozote.

XS
SM
MD
LG