Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Oktoba 11, 2024 Local time: 00:02

Kiongozi wa zamani kwenye Baraza la Seneti la Marekani, Harry Reid afariki dunia


Seneta wa zamani wa Marekani, Harry Reid kwenye kongomano la chama cha Democratic, Nevada, Marekani
Seneta wa zamani wa Marekani, Harry Reid kwenye kongomano la chama cha Democratic, Nevada, Marekani

Kiongozi wa zamani wa walio wengi kwenye baraza la Seneti  Mdemocrat Harry Reid mmoja kati ya maseneta waliohudumu miaka mingi, amefariki nyumbani kwake katika mji wa Henderson jimbo la Nevada, akiwa na umri wa miaka 82.

Mke wake Landra Reid alisema mume wake alifariki kwa amani Jumanne baada ya kupambana kwa miaka minne na saratani ya kongosho.

Mwanamasumbwi huyo wa zamani aliyegeuka mwanasheria alitambuliwa na wengi kama mmoja wa wabunge wanaofikia makubaliano ndani ya bunge.

Katika kipindi cha miaka 34 kama seneta, Reid alifanya mazungumzo ya siri siri kumaliza malumbano ya kisiasa, na alikuwa na mchango mkubwa kwa kufanya baraza la Seneti lidhibitiwe na chama chake cha Democratic kupitia marais wawili. Kuzorota kwa uchumi wa Marekani, kulipelekea chama cha Republican kudhibiti bunge baada ya uchaguzi wa mwaka 2010.

Alistaafu mwaka 2010. Rais Joe Biden alisema katika taarifa baada ya kifo cha mwenzake wa muda mrefu katika Seneti, “kama Harry aliahidi kufanya jambo, atalifanya".

XS
SM
MD
LG