Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 03:03

Kesi ya uchaguzi dhidi ya Barrow yatupiliwa mbali Gambia


Rais wa Gambia Adama Barrow baada ya ushindi wake mapema Decemba

Mahakama ya juu ya Gambia Jumanne ipetupilia mbali kesi iliowasilishwa dhidi ya ushindi wa rais Adama Barrow kwa madai kwamba walioiwasilisha hawakufuata hatua za kisheria, kama  inavyohitajika.

Barrow alishinda tena kwenye uchaguzi wa Decemba 4 kwa asilimia 53 ya kura zilizopigwa akifuatiwa na mpinzani wake wa karibu Ousainou Darboe kwa asilimia 28 ya kura, wakati wagombea wengine wawili wakipinga matokeo kwa madai kwamba kulikuwa na dosari kwenye vituo vya kupigia kura, bila kutoa ushahidi.

Kwa mijibu wa shirika la habari la Reuters, chama cha Darboe cha United DiplomaticUDP,kiliwasilisha ombi la kufutwa kwa zoezi hilo, kwenye mahakama ya juu kwa madai kwamba halikufanyika kwa njia ya haki. Hata hivyo mahakama imesema kwamba chama hicho hakikuwasilisha malalamishi hayo ndani ya siku 5 kwa Barrow kama inavyohitajika kwenye sheria za Gambia.

XS
SM
MD
LG