Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 12:49

Askofu Desmond Tutu kuzikwa siku ya mwaka mpya


Ofisi ya jiji la Capetown Afrika Kusini, iliwashwa kwa rangi ya zambarau Jumapili, Desemba 26, 2021, kwa kumbukumbu ya Askofu Mkuu wa Kianglikana Desmond Tutu.
Ofisi ya jiji la Capetown Afrika Kusini, iliwashwa kwa rangi ya zambarau Jumapili, Desemba 26, 2021, kwa kumbukumbu ya Askofu Mkuu wa Kianglikana Desmond Tutu.

Raia wa afrika Kusini wamekuwa walitembelea kanisa la St Georges mjini  cape town kutoa heshima zao za mwisho kwa Askofu mkuu Desmond Tutu aliyefariki jumapili

Raia wa afrika Kusini wamekuwa walitembelea kanisa la St Georges mjini cape town kutoa heshima zao za mwisho kwa Askofu mkuu Desmond Tutu aliyefariki jumapili.

Ukumbi wa manispaa wa Cape Town na baadhi ya sehemu ya Table Mountain zilipambwa kwa rangi za hudhurungi kwa ajili ya kuheshimu Maisha ya Tutu. Jumatano Dayosisi ya Pretoria na baraza la makanisa la Afrika Kusini watafanya ibada katika mji wa Pretoria.

Siku hiyo hiyo , Cape Town nayo inatarajiwa kufanya sherehe ya dini mbalimbali, mwili wa marehemu Tutu utalazwa kwa ajili ya kumbukumbu katika kanisa la St.Georges mjini cape town Ijumaa kabla ya ibada kubwa ya kumuaga kufanyika Jumamosi.

Mtetezi huyo wa ubaguzi wa rangi atapewa mazishi ya kiwango cha kwanza kukiwa na matukio mbalimbali ya kidini. Mazishi yake yatafanyika siku ya mwaka mpya , Januari mosi mwaka 2022.

XS
SM
MD
LG