Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 11:24

Marekani yaunga mkono juhudi za waziri mkuu Somalia za uchaguzi wa haraka na kuaminika


Waziri Mkuu wa Somalia Mohamed Hussein Roble alipongumza katika bunge mjini Mogadishu,
Somalia, September 23, 2020.
Waziri Mkuu wa Somalia Mohamed Hussein Roble alipongumza katika bunge mjini Mogadishu, Somalia, September 23, 2020.

Marekani imesema jaribio la kumsimamisha kazi Waziri Mkuu wa Somalia Mohammed Hussein Roble lilikuwa la kustusha na kwamba inaunga mkono juhudi zake za uchaguzi wa haraka na wa kuaminika.

Marekani imesema jaribio la kumsimamisha kazi Waziri Mkuu wa Somalia Mohammed Hussein Roble lilikuwa la kustusha na kwamba inaunga mkono juhudi zake za uchaguzi wa haraka na wa kuaminika.

Idara ya Masuala ya Afrika ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilisema katika ukurasa wake wa Twitter Jumatatu jioni kwamba iko tayari kuchukua hatua dhidi ya wale wanaozuia njia ya amani ya Somalia.

Siku ya Jumatatu, Rais Mohamed Abdullahi Mohamed alisema amesitisha mamlaka ya Roble kwa tuhuma za ufisadi, hatua ambayo waziri mkuu aliitaja kuwa jaribio la mapinduzi, na kuzidisha mzozo wa madaraka kati ya viongozi hao wawili.

Jaribio la kusimamishwa kwa Roble linatisha na tunaunga mkono juhudi zake za uchaguzi wa haraka na wa kuaminika, ofisi hiyo ilisema. Pande zote lazima zijiepushe na vitendo na kauli za kuongeza mvutano.

Rais Mohamed alimshutumu Roble kwa kuiba ardhi inayomilikiwa na Jeshi la Kitaifa la Somalia (SNA) na kuingilia uchunguzi wa wizara ya ulinzi.

XS
SM
MD
LG