Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Februari 06, 2023 Local time: 16:16

Kesi za ngono zilizo kwama zaanza kusikilizwa Uganda


Moja ya kampeni dhidi ya unyanyasaji wa majumbani

Mahakama kote nchini Uganda imeanza kusikiliza mamia ya kesi za ghasia za ngono zilizokwama kwa muda mrefu zikiwemo kesi nyingi zinazohusiana na ubakaji wa watoto, ikiwa ni juhudi za kutekeleza haki kwa waathiriwa.

Kulingana na Jaji wa Mahakama Kuu Gadenya Paul Wolimbwa, anaye ratibu mradi huo, majaji 40 kwenye mahakama 13 katika miji 6 wanalenga kusikiliza kesi 700 za unyanyasaji wa kingono, katika kipindi cha siku 40.

Jaji Wolimbwa anaeleza kuwa katika Mahakama Kuu kwa mfano, kati ya kila kesi kumi zinazo wafikia majaji, 6 kati ya kesi hizo zina husiana na unyanyasaji wa kingono.

Anaeleza kuwa kesi hizo zinahusiana na ubakaji, utekaji nyara kwa ajili ya kutaka kubaka, unyanyasaji na nyenginezo.

Ghasia za kingono ni vitendo vya uhalifu vinavyofanyika zaidi huko Uganda.

Takwimu rasmi za serikali zinaonyesha kuwa kuna zaidi ya kesi laki mbili elfu kumi zilizo ripotiwa kati ya 2015 hadi 2016.

Na ripoti ya shirika linalo shughulikia watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF, iliyotolewa mwezi ogusti imegundua kwamba kati ya kila watoto watatu wa Uganda, mmoja amekabiliwa na shambulio la kingono.

Vikao maalum vya kesi hizo zimeanza kusikiliza Jumatatu kwa lengo la kupunguza zaidi ya kesi elfu sita za unyanyasaji wa kingono ambazo hazijasikilizwa bado.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG