Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 28, 2024 Local time: 05:14

Oxfam yachunguza shutma mpya za ngono


Winnie Byanyima
Winnie Byanyima

Shirika la hisani la Oxfam limesema linachunguza dazeni ya shutuma mpya za manyanyaso ya ngono.

Hii inafuatia ripoti ya hivi karibuni kwamba baadhi ya wafanyakazi wa shirika hilo nchini Haiti waliwalipa fedha makahaba katika kipindi cha baada ya tetemeko la ardhi la mwaka 2010 nchini humo.

Oxfam ni moja ya mashirika ya misaada yanayojulikana sana duniani kwa shughuli zake za kupunguza umaskini na kutoa misaada ya dharura. Lakini madai ya manyanyaso ya ngono yanatishia kuharibu juhudi zote ambazo zimefikiwa na shirika hilo.

Wakuu wa Oxfam wameomba msamaha Jumanne kwa uharibifu uliosababishwa na kusema kwamba kesi nyingine 26 zinafanyiwa uchunguzi hivi sasa.

Mkurugenzi mtendaji wa Oxfam International, Winnie Byanyima anasema, “hii inahusu sera za Oxfam na watu wetu. Baadhiya watu wenye nia mbaya walikuja kwenye taasisi yetu na kusaliti imani wa watu wa Uingereza. Lakini walifanikiwa kupewa barua za kuwataka waondoke. Ni makosa makubwa. Kwahiyo tutabadili jinsi tulivyozoea kufanya mambo yetu.”

Aliyekuwa mkurugenzi wa kutoa huduma za misaada nchini Haiti, Ron Van Hauwermeiren wakati madai yalipotolewa amekana kuhusika katika kashfa hiyo na amekubaliwa kujiuzulu kabla ya uchunguzi kukamilika.

Hauermeiren anasema, “ilikuwa ni jambo lakiungwana. Ilikuwa ni kama vile nilikuwa nakutana na mwanamke na kushirikiana naye kimapenzi nchini Ubelgiji. Kwa sasa nina mpenzi hapa na nitapendana naye. Hakuna kosa lolote kwa kufanya hivyo”

Kufuatia kashfa hiyo, mashirika mengine ya kutoa misaada yameanza kuwachunguza wafanyakazi wake na jinsi wanavyoshughulikia tuhuma za ngono, huku serikali kadhaa zikiangazia uhusiano wao na mashirika hayo. Gemma Houldey, alikuwa mfanyakazi wa kutoa misaada na sasa ni mtafiti kuhusu sekta hiyo.

“Mazingira ya kufanya kazi yamekuwa yakiwazuia wanaonyanyaswa kingono kuzungumza hadharani au hata kuripoti dhuluma kama hizo kutokana na uhusiano kati ya yuleanayetoa msaada na anayepokea. Uhusiano huo unapokosa kuheshimiwa, basi kinachofuatia ni picha mbaya sana kuhusu sekta nzima,” anasema Houldey.

Shirika la Oxfam lilipokea kiasi cha dola milioni 45 kutoka kwa serikali ya Uingereza mwaka 2017, na kiasi sawa na hicho kutoka Umoja wa Ulaya (EU). Wafadhili wote wawili kwa sasa wanatathmini ufadhili wao.

Waziri wa nchi wa masuala ya maendeleo ya kimataifa wa Uingereza, Penny Mordaunt anasema’ “kama humpi ulinzi kila mtu ambaye anawasiliana na taasisi yako, ikiwemo wale wanaofaidika na misaada, wafanyakazi na watu wa kujitolea basi hatukupi ufadhili.”

Oxfam linasema kwamba wafadhili wa kawaida 7,000 wamesitisha misaada katika siku 10 zilizopita.

Waathirika wa manyanyaso katika sekta ya misaada wameanza kuzungumza, hatuahii inakaribishwa na wengi duniani. Lakini kuna hofu kwamba ufadhili wa kifedha kwa shirika hilo utapunguzwa wakati dunia inakabiliwa na mizozo kadhaa ya kibinadamu.

XS
SM
MD
LG