Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 30, 2023 Local time: 23:02

Mkuu wa zamani wa Oxfam akiri kufanya makosa


maeneo yanayokabiliwa na unyanyasaji wa ngono duniani

Mkurugenzi wa zamani wa shirika la hisani la Oxfam ambaye yuko katikati ya kadhia za manyanyaso ya ngono amesema Alhamisi amefanya makosa wakati alipokuwa akifanya kazi nchini Haiti.

Lakini kiongozi huyo amekanusha kulipia ngono kwa makahaba au kuwanyanyasa watoto wadogo.

Katika majibu yake ya kwanza juu ya shutuma kwa tabia yake, Roland Van Hauwermeiren amesema katika barua yake ya wazi kwa shirika la utangazaji nchini Ubelgiji anakotokea kuwa hataki kujifanya ni muathirika lakini anakhofia kwamba Oxfam, wafanyakazi wengine wa misaada na wale ambao wanawasaidia wasitaabishwe na shutuma za uongo.

Katika barua yake ya kurasa nne ambayo shirika la habari la Reuters wameiona, amemshutumu mfanyakazi mmoja wa zamani ambaye hakumtaja jina kuwa ni chanzo cha ripoti ambazo zimetikisa jamii inayoshughulikia masuala ya kibinadamu ulimwenguni na kuichochea Uingereza na Umoja wa Ulaya (EU) kutathmini ufadhili kwa Oxfam.

“Mimi si mtakatifu. Mimi ni mtu wa kawaida na nimefanya, si rahisi kukubali na nimepata aibu kubwa,” mwanajeshi huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 68 aliandika kwa lugha ya shirika la utangazaji la Uholanzi VTM.

Amesema alijiuzulu wadhifa wake wa kusimamia shughuli za Oxfam baada ya tetemeko la ardhi la mwaka 2010 nchini Haiti kwasababu alishindwa kuwa na udhibiti unaokubalika kwa wafanyakazi wake ambao walishutumiwa kwa vitendo vya ngono. Lakini amekanusha yeye mwenyewe kufanya makosa yoyote – hajawahi kuandaa “tafrija za ngono” au kutembelea madanguronchini humo.

Amekitri kuwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi kwa muda mfupi na mwanamke mmoja wa Haiti ambaye alikutana naye ikiwa ni matokeo ya kumpa mdogo wake maziwa ya unga na nepi kwa ajili ya mtoto wake.

Amekanusha kumpa mwanamke huyo pesa lakini mahusiano yao yamechochea uvumi huo.

XS
SM
MD
LG