Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 27, 2022 Local time: 01:20

Ripoti ya UN yathibitisha uhalifu zaidi ulifanyika Burundi


Burundi

Ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu iliyotolewa Jumatano inaeleza kuwa uhalifu zaidi dhidi ya ubinadamu ulifanyika nchini Burundi, mwaka 2017 na 2018 na kuelezewa kwa ufasaha na maafisa wa juu wa UN.

Burundi imejaribu nakushindwa kuizuia tume ya uchunguzi ya UN kwa burundi, iliyoundwa na baraza la haki za binadamu la umoja huo mwaka 2016 na kukataa kabisa kuipa ushirikiano.

Tume hiyo ilisema mwaka 2017 kwamba maafisa wa ngazi ya juu walihusika kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu tume ina misingi thabiti kuamini kwamba uhalifu dhidi ya ubinadamu unaendelea kutendwa nchini burundi, ripoti ya tume ya hivi karibuni imebaini.

Uhalifu huo unajumuisha mauaji, kuwekwa kizuizini au kunyimwa haki nyingine za msingi uhuru, mateso, ubakaji na aina nyingine za manyanyaso ya ngono. Msemaji wa rRais pierre nkurunziza na waziri wa haki za binadamu nchini Burundi amekataa kutoa maoni kuhusu ripoti hiyo.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG