Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 03, 2024 Local time: 15:46

Bill Cosby ahukumiwa miaka 3-10 gerezani


Bill Cosby
Bill Cosby

Mcheza sinema na mchekeshaji maarufu nchini Marekani Bill Cosby amehukumiwa kwenda gerezani kati ya miaka mitatu hadi kumi na mahakama ya jimbo la Pennsylvania baada ya kukutwa na hatia mwezi April, 2018 katika kosa la udhalilishaji wa kingono.

Cosby aliyekuwa akikabiliwa na mashitaka kadha yaliyotokana na madai ya wanawake wengi alikutwa na hatia mwezi Aprili mwaka huu katika makosa matatu ya udhalilishaji wa kingono kwa kumpa dawa na kumfanyia tendo la ngono Andrea Constand mwaka 2004.

Bill Cosby akitoka mahakamani Aprili 2018 baada ya kukutwa na hatia
Bill Cosby akitoka mahakamani Aprili 2018 baada ya kukutwa na hatia

Mawakili watetezi wa Cosby, mwenye umri wa miaka 81, walionyesha dalili awali kuwa watakata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.

XS
SM
MD
LG