Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 14, 2024 Local time: 10:20

Jinsi matapeli wa Nigeria walivyowaibia watu, makampuni mamilioni ya fedha


Maafisa wa Idara ya Makosa ya Jinai wa serikali kuu wanamshikilia mahabusu, wapili kutoka kushoto, mjini Los Angeles baada ya kufanya msako wa alfajiri ambao ulipelekea darzeni za watu kukamatwa Agosti 22, 2019. Wengi wa washtakiwa hao ni raia wa Nigeria.
Maafisa wa Idara ya Makosa ya Jinai wa serikali kuu wanamshikilia mahabusu, wapili kutoka kushoto, mjini Los Angeles baada ya kufanya msako wa alfajiri ambao ulipelekea darzeni za watu kukamatwa Agosti 22, 2019. Wengi wa washtakiwa hao ni raia wa Nigeria.

Kwa miaka kadhaa darzeni za matapeli kutoka Nigeria na nchi nyingine wamekuwa wakiwaibia watu binafsi na wafanyabiashara mamilioni ya dola za Kimarekani, wakipitisha fedha hizo za wizi kupitia akaunti zilizokuwa zinaendeshwa na “madalali” wawili wenzao kutoka Nigeria waliokuwa wanaishi Los Angeles.

Wakati biashara hiyo ya utapeli ikiendelea kukua katika mazingira ya ujangili, raia wa Nigeria Valentine Iro na Chukwudi Christogunus Igbokwe walikuwa maarufu wakishughulika na uhalifu huo na kutumia majina ya bandia, likiwemo “Iro Enterprises” na “Chris Kudon.”

Kati ya mwaka 2014 na 2018, Iro na Igbokwe, wakishirikiana na matapeli wa kimataifa wengine 80, walisaidia mtiririko wa miradi ya utapeli iliyopelekea kuibiwa siyo chini ya dola za Marekani milioni 6 na jaribio la wizi wa zaidi ya milioni 40 kutoka kwa waathirika wa utapeli huo kutoka zaidi ya nchi 10, kwa mujibu wa mashtaka 252 yaliyofunguliwa na serikali kuu Alhamisi.

Matapeli hao waliwaumiza watu binafsi na kuziathiri biashara ndogo ndogo na kubwa.

Katika kuwalenga wafanyabiashara, walitumia mbinu maalum inayoitwa “udukuzi wa email za biashara,” ambazo pia zinajulikana kama CEO fraud.

Katika mpango wa utapeli huo, tapeli wa mitandao hupata fursa kudukua ndani ya mfumo wa kompyuta ya kampuni na kisha, kujifanya kama ni mtendaji wa kampuni, na kumlaghai mfanyakazi kuhamisha fedha kinyume cha sheria kupeleka katika akaunti ya benki ambayo matapali walikuwa wanaimiliki.

Mashtaka hayo yameorodhesha waathirika wa utapeli katika makampuni kadhaa.

Mnamo mwaka 2014, Msambazaji wa nguo kutoka San Diego alituma takriban dola za Marekani 46,000 kwenda kwenye akaunti ya benki iliyokuwa inamilikiwa na tapeli mmoja wapo, wakiamini walikuwa wanamlipa mfanyabiashara wa China wakiagiza mashati ya kiume.

Mwaka 2016, kampuni moja ya Texas iliyokuwa haijatambuliwa ilitapeliwa kutuma dola za Marekani 187,000 kwenda kwenye akaunti ya wizi. Kampuni hiyo ilifikiria kuwa inafanya malipo kwa ajili ya kununua mashine ya kukamua mafuta.

Hujuma hii pia iliwalenga watu wazee na waathirika wa utapeli wa kimapenzi.

Kwa mfano, mwaka 2016 mwanamke wa Kijapani, aliyetajwa katika nyaraka za mahakama kama F.K, alipoteza zaidi ya dola za Marekani 200,000 katika miezi kumi ya utapeli wa kimapenzi kwa kutapeliwa na mtu aliyejifananisha na kapteni wa jeshi la Marekani aliyeko Syria.

Mwaka 2017, mwanaume, 86, mwenye maradhi ya kupoteza kumbukumbu alituma karibu dola za Marekani 12,000 kwenye akaunti ya benki iliyokuwa inamilikiwa na tapeli mmoja.

Idara ya Sheria iliwasilisha mashtaka mara baada ya kuwakamata watu 14, akiwemo Iro na Igbokwe, mapema Alhamisi,

Watu wengine watatu walikuwa tayari wako rumande. Washtakiwa sita wako nchini Marekani bado hawajakamatwa, wakati vyombo vya serikali vinafanya kazi na washirika wake katika nchi nyingine tisa kuwakamata watuhumiwa wengine 57, wengi wao inaaminika wako nchini Nigeria.

XS
SM
MD
LG