Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 05, 2024 Local time: 21:22

Uchaguzi wa Rais 2019 :Buhari akabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa mpinzani wake Abubakar


 Atiku Abubakar
Atiku Abubakar

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari na mpinzani wake Atiku Abubakar wanaendelea na kampeni iliyokuwa na mchuano mkali katika sehemu mbalimbali za nchi kuelekea uchaguzi wa Februari 16.

Buhari, ni wa chama kinachotawala cha APC na mpinzani aliyewahi kuwa makamu Atiku Abubakar ni wa chama cha People’s democratic party – PDP.

Uchaguzi mkuu wa Nigeria unawagombea 60 wa urais, japo nafasi yao ya kushinda ni ndogo sana.

Mali na ushawishi wa kisiasa kati ya vyama vikuu vya kisiasa vyenye ushawishi na ushindani mkubwa ndio vigezo vikubwa katika siasa za Nigeria, nchi yenye utajiri mkubwa wa mafuta na idadi kubwa ya watu barani Afrika.

Jumamosi, wakati wa mkutano wa kisiasa mjini Lagos, Buhari aliwaambia maelfu ya wafuasi wake kwamba ataendelea kutimiza ahadi alizotoa wakati wa uchaguzi wa mwaka 2015.

Buhari anaendeleza ahadi ya kupambana na ufisadi, kuimarisha ukuaji wa uchumi na kuimarisha usalama.

Serikali yake Buhari inakabiliwa na changamoto kubwa ya usalama kutoka kwa makundi ya wapiganaji wa Boko Haram na Islamic state huku hali ya umasiki ikiendelea kuongezeka.

Wapinzani wake wanasema serikali imeshindwa kukabiliana na ufisadi na kuwalenga tu maadui wake, huku ikikosa kukabiliana na madai yanayohusu washirika wake, katika vita dhidi ya ufisadi.

Amnesty international na watetezi wa haki za kibinadamu nao wanashutumu jeshi la Nigeria kwa ukandamizaji wa haki za kibinadamu, ikiwemo mauaji ya waandamanaji. Lakini jeshi likitetea matumizi ya nguvu.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Washington, DC

XS
SM
MD
LG