Upatikanaji viungo

Breaking News

Nigeria yatupilia mbali malalamiko yaliyo tolewa na Marekani, Uingereza, EU


Rais Muhammadu Buhari

Serikali ya Nigeria imeonya mataifa mengine kuacha kuingilia kati mambo yake ya ndani, “ikisistiza kuwa nchi hiyo ya Afrika Magharibi itafanya “uchaguzi ulio huru, wa haki” wa nafasi ya urais ifikapo Februari 16.

Akijibu wasiwasi ulioelezewa na Marekani, Uingereza na Umoja wa Ulaya kwa kitendo cha Rais Muhammadu Buhari kumsimamisha kazi Jaji Mkuu, msemaji wa rais ametetea uamuzi huo.

Serikali Kuu ya Nigeria “imedhamiria kuhakikisha uchaguzi huru, wa haki unafanyika. Serikali hii haiwezi kupindisha kanuni na haitaruhusu yeyote kuingiliwa kati mambo yetu,” msemaji Garba Shehu amesema katika tamko lililotolewa jioni Jumamosi, Shirika la Habari la Reuters limeripoti.

Baraza la Seneti la Nigeria limepanga kikao cha dharura Jumanne, na moja ya ajenda ni kusimamishwa kazi kwa jaji mkuu, gazeti la Punch lenye makao yake Lagos limeripoti Jumapili.

Baraza la wawakilishi limeahirishwa hadi Februari 19, baada ya uchaguzi wa rais na Bunge la Taifa.

Katika tamko lililofuatia Jumapili jioni, msemaji huyo alizielezea serikali hizo tatu za kigeni kama ni “marafiki” lakini amesema ukosoaji wao “unaelekea kusukumwa na dhana zisizoweza kuthibitishwa na, kwa kweli, na aina fulani ya kiburi dhidi ya demokrasia hii ya Kiafrika. …Hakuna nchi yeyote kati ya nchi zenu ambayo itaruhusu mtu aliyenasa katika utata wa kisheria kuongoza mfumo wa sheria mpaka pale atakapo kuwa amekutikana hana makosa.”

Tamko hilo refu lilikusudia kufafanua uamuzi wa Buhari kumsimamisha kazi Jaji Mkuu Walter Onnoghen kwa madai ya kutoa maelezo ya uongo juu ya mali zake.

Buhari amesema hatua hiyo inatokana na ombi la Mahakama ya Maadili iliyokuwa imeanza kusikiliza kesi dhidi ya Onnoghen wiki iliyopita. Mahakama ya Rufaa imeamuru kesi hiyo kusimamisha Alhamisi.

Ibrahim Tanko Mohammed, ambaye ni jaji wa ngazi ya juu katika nafasi ya pili kimadaraka aliapishwa kuwa kaimu jaji mkuu Ijumaa.

Wakati huohuo Kikundi cha Jumuiya ya Kiraia cha Nigeria, ambacho kinawakilisha zaidi ya vikundi 70 ambavyo vinashirikiana kusaidia uchaguzi ulio wa haki, na uwazi umetoa tamko ukimsihi Buhari “kubadilisha maamuzi yake ambayo ni kinyume cha katiba na kinyume cha sheria na kuacha kabisa kuingilia kati uhuru wa mahakama…”

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG