Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 21, 2024 Local time: 07:02

VOA yaadhibu wafanyakazi 15 wa Idhaa ya Hausa


Ramani ya Afrika
Ramani ya Afrika

Sauti ya Amerika imewaachisha kazi au imependekeza kuwaondoa kazini wafanyakazi 15 katika idhaa ya Hausa, kufuatia shutma za vitendo visivyo stahili, ikiwemo kupokea malipo batili.

Mkurugenzi wa VOA Amanda Bennett amesema katika barua pepe kwa wafanyakazi Alhamisi kwamba uongozi wa VOA ulipewa taarifa juu ya shutuma hizo “miezi ya hivi karibuni” na kuanzisha uchunguzi kadhaa.

“Wakati sheria za kulinda faragha ya mtu zinatuzuilia kutoa ufafanuzi zaidi juu ya wafanyakazi hawa, ni baada ya kumalizika uchunguzi huo ndio hatua hii ya kuwaachisha kazi au pendekezo la kuwaondoa kazini linafanyika,” amesema Mkurugenzi huyo.

Idhaa ya Hausa VOA inatangaza nchini Nigeria na Niger na huangaza kwa kina matukio ya eneo hilo la Afrika.

Bennett amesema malipo yasiyo halali yalifanywa “na afisa wa eneo ambako matangazo yanapeperushwa.”

“Uchunguzi tofauti umeanzishwa ili kujua kama matangazo yoyote ya VOA yalishawishiwa kwa njia isiyo kubalika,” amesema Mkurugenzi. “Iwapo ushawishi huo utagundulika, tutachukuwa hatua mara moja na kwa uwazi.”

Bennett amesema uongozi wa VOA Kitengo cha Afrika kimetoa ushirikiano kamili katika uchunguzi huu na kusaidia katika kufikia maamuzi ya kuwaachisha kazi au kuwaondoa kazini wafanyakazi husika.

“Uongozi wa Kitengo hicho, kama sisi wote, wanahima ya hali ya juu katika kufuata maadili na hawawezi kuvumilia aina yoyote ya uvunjaji wa sheria,” amesema.

Mkurugenzi ameongeza kuwa : “Hakuna kitu muhimu zaidi hapa VOA kuliko kitendo cha kuaminiwa na wasikilizaji wetu. Ili kuendeleza uaminifu huo, hakuna kitu muhimu zaidi kuliko kuendeleza iwezekanavyo viwango vya juu vya ukweli katika uandishi, taaluma, sheria na maadili.”

XS
SM
MD
LG