Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 07, 2024 Local time: 02:53

VOA yalaani kufungiwa matangazo yake Burundi


Rais Pierre Nkurunziza
Rais Pierre Nkurunziza

Sauti ya Amerika imelaani kitendo cha hivi karibuni cha serikali ya Burundi kufungia matangazo yake kwa miezi sita, kuanzia Mei 7, 2018.

"Tumesikitishwa na kitendo cha Baraza la Mawasiliano ya Taifa la Burundi kupiga marufuku VOA kutangaza programu zake za habari," amesema Mkurugenzi wa VOA Amanda Bennett katika tamko lake rasmi.

"Wasilikilizaji wetu wanategemea kupata habari za ukweli kutoka VOA, ripoti za matukio ambayo yana malengo bila ya upendeleo wa upande wowote, na kwa hiyo katazo hili linawanyima wananchi wa Burundi kupata habari kutoka katika chanzo cha kuaminika katika wakati huu muhimu nchini humo. Hili linashitusha zaidi kwa kuwa limefanyika siku moja baada ya maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Habari Duniani- siku ambayo imetoa wito kwa serikali kuondosha na sio kuweka pingamizi dhidi ya vyombo vya habari."

"Maudhui ya matangazo ya VOA yataendelea kupatikana katika lugha ya Kirundi na Kinyarwanda kupitia matangazo ya masafa mafupi, katika Interneti na mitambo ya FM iliyoko nchi jirani," imesema taarifa hiyo.

Siku ya Ijumaa Burundi ilitangaza kuvifungia kwa miezi sita vituo viwili vya utangazaji – Sauti ya Amerika na Idhaa ya BBC, wiki mbili kabla ya nchi hiyo kupiga kura ya pendekezo la kurekebisha katiba ya nchi hiyo, ikiwemo mabadiliko ya kikomo cha muhula wa urais.

Kufungiwa kwa vituo hivyo kumetangazwa Ijumaa na Baraza la Mawasiliano laTaifa la Burundi, ambalo limeituhumu VOA na BBC kwa kuvunja sheria za utangazaji zinazosimamia vyombo vya habari na kujihusisha na vitendo ambavyo ni kinyume cha maadili.” Tamko hilo la serikali limesema kuwa kufungiwa huko kutaanza Jumatatu.

VOA ina mitambo miwili ya FM ya kutupia matangazo nchini Burundi ambavyo kunauwezekano na vyenyewe kufungiwa iwapo serikali itaendelea na marufuku hiyo. Lakini, wasikilizaji wanaweza kusikiliza matangazo ya VOA katika matangazo ya masafa mafupi, au kwa kutumia mitambo ya kupeperusha matangazo ya FM zilizoko nchi za jirani- Congo au Rwanda.

Burundi itaendesha kura ya maoni juu ya katiba Mei 17 ambayo itaiwezesha kuongeza muhula wa urais kutoka miaka mitano hadi saba. Katiba hiyo itaendelea kumzuia rais kutawala kwa mihula miwili, lakini wafuasi wa Rais Pierre Nkurunziza amesema kura ya “ndio” italeta mabadiliko na kumruhusu agombanie kwa mihula miwili zaidi.

Nkurunziza ameiongoza nchi hiyo ya Afrika ya Kati kuanzia mwaka 2005.

Marekani ilimkosoa vikali Rais kwa kutaka kujiongezea muhula wa tatu mwaka 2015, na hivi karibuni ili laani madai ya vitendo vya uvunjifu wa amani na vitisho dhidi ya wapinzani wanaodai kuwepo kura hiyo ya maoni.

XS
SM
MD
LG