Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 26, 2020 Local time: 12:55

Buhari atarajiwa kurejea Nigeria - Msemaji wa rais


Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari (Kulia) anatarajiwa kurudi nchini baada ya kupokea matibabu nchini Uingereza.

Msema ji wa rais wa Nigeria, alitangaza kupitia taarifa siku ya Jumamosi kwamba kiongozi huyo atarudi nyumbani baada ya kuwa nje ya nchi kwa kipindi kirefu akipokea matibabu ya ugonjwa ambao haujatangazwa hadharani.

Rais Muhammadu Buhari amekuwa mjini London, Uingereza, tangu tarehe 7 mwezi Mei, na baadhi ya Wanigeria walikuwa wameanza kumtaka arejee kazini au ajiuzulu.

Buhari aliondoka Nigeria mnamo mwezi Julai mwaka huu ili kupata matibabu mjini London, ambako alikaa kwa muda wa miezi miwili kabla ya kurudi nnyumbani mnamo mwezi Machi.

Lakini aliondoka tena mapema mwezi Mei. Wakati akiwa nje ya nchi, Buhari alikabidhi baadhi ya mamlaka ya uongozi kwa makamu wake, Yemi Osinbajo. Taarifa iliyotangaza kurejea kwa rais huyo ilisema kuwa atahutubia Wanigeria kupitia matangazo ya moja kwa moja Jumatatu asubuhi.

Facebook Forum

Kura ya Maoni : Uchaguzi Tanzania

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

XS
SM
MD
LG