Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 04:00

Trump na Buhari wajadili ugaidi, uchumi


Rais Donald Trump (kulia) akiwa katika mazungumzo na Rais Muhammadu Buhari
Rais Donald Trump (kulia) akiwa katika mazungumzo na Rais Muhammadu Buhari

Rais wa Marekani Donald Trump amejaribu kuboresha mahusiano yake na Afrika Jumatatu, wakati akimkaribisha mgeni wake Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari.

Buhari ni kiongozi wa kwanza wa nchi za Afrika zilizoko Kusini mwa jangwa la Sahara kufanya mkutano na Trump Ikulu ya Marekani- White House.

Trump alikosolewa kwa kuripotiwa kutoa maoni yanayo idhalilisha Afrika.

Wakati akitoa maoni yake kwa umma akiwa na Buhari, Trump alijikita zaidi katika kuelezea malengo ya pamoja na maslahi ya pande mbili, kama vile kupambana na ugaidi na kuongeza biashara kati ya nchi hizi mbili.

“Tunapenda helikopta – pia yeye anazipenda zaidi yangu,” Trump alifanya mashara, wakati akieleza uamuzi wa serikali yake wa kuidhinisha makubaliano ya mauzo ya vifaa vya kijeshi venye thamani ya Dola za Kimarekani $600 kwa Nigeria.

XS
SM
MD
LG