Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 28, 2022 Local time: 15:10

Uchaguzi Mkuu Nigeria 2019 : Faida na madhara ya kuahirishwa uchaguzi


Afisa wa polisi akilinda vifaa vya uchaguzi katika ofisi za Tume Huru ya Uchaguzi, Kano, Kaskazini mwa Nigeria, Feb. 16, 2019.

Uamuzi wa dakika ya mwisho kuchelewesha uchaguzi mkuu nchini Nigeria, ambao hivi sasa umepangwa kufanyika Jumamosi, umesababisha shaka juu ya ahadi ya kuwepo uchaguzi huru na wa haki katika nchi yenye watu wengi zaidi Afrika.

Kwa wananchi wa Nigeria, ni hatua isiyopendeza, ingawaje sio kitu kigeni. Nchi hiyo haijawahi kufanya uchaguzi wa rais kwa wakati uliopangwa tangu mwaka 2007, wakati rais mstaafu Umaru Yar’Adua alipomshinda Rais Muhammadu Buhari kwa urahisi.

Lakini kucheleweshwa uchaguzi sio jambo lenye kuleta wasiwasi kwa Nigeria peke yake.

Uchambuzi wa takwimu

Katika Bara la Afrika, chaguzi za rais 27 kati ya 102 zimekuwa zikicheleweshwa tangu mwaka 2009, kwa mujibu wa takwimu zilizochambuliwa na Sauti ya Amerika –VOA, kutoka katika ripoti mbalimbali na kutoka katika Taasisi ya Uchaguzi kwa Ajili ya Kunedeleza Democracy Afrika (Electoral Institute for Sustainable Democracy in Africa(( https://www.eisa.org.za/ )), asasi isiyokuwa ya kibiashara yenye makao yake Johannesburg, Afrika Kusini, inayohamasisha chaguzi kuwa za haki.

Nchi 20 kati ya 51 kati ya zile zilizofanya uchaguzi wa rais wameshuhudia kuahirishwa uchaguzi mara moja au zaidi katika kipindi cha miaka 10. Ucheleweshaji huo ulikuwa kati ya siku mbili hadi miaka kadhaa, wakati nyingi katika hizo zikicheleweshwa angalau kwa wiki kadhaa. Ivory Coast ilikuwa na ucheleweshaji wa muda mrefu zaidi – miaka mitano.

Sababu za kuahirishwa uchaguzi

Sababu kubwa za kuahirishwa uchaguzi zinatofautiana, ikiwemo vita vya wenyewe kwa wenyewe na uasi na pia maafa na hata maafisa kujaribu kubadilisha muda wa katiba wa kushikilia madaraka. Wakati mwengine, tarehe za uchaguzi zinabadilishwa kutokana na maandalizi kuwa na mapungufu.

Wakati nchi ikiwa haiwezi kufanya uchaguzi kama ulivyopangwa, inaweza kuathiri uhalali wa mchakato mzima. Nchini Nigeria, wapiga kura wameiambia VOA walikuwa wamebabaishwa na ucheleweshaji huu na inawapa shaka.

(( https://www.voanews.com/a/nigeria-delays-national-elections-by-one-week-/4789593.html )).

Lakini uchambuzi wa VOA unaonyesha kuwa kuahirishwa kwa uchaguzi sio dalili ya uongozi mbovu kwa tukio hilo tu – kwani, mara nyingi demokrasia imara na dhaifu zinakuwa na ucheleweshaji uchaguzi mara chache.

Ucheleweshaji na Demokrasia
Kila mwaka Kitengo cha Economist Intelligence, cha kampuni inayochapisha gazeti la Economist newspaper, ilitoa Jadwali la Demokrasia ((https://www.eiu.com/topic/democracy-index )). Jadwali hilo linaonyesha nchi na daraja zao katika vigezo kama vile mchakato wa uchaguzi, ushiriki wa kisiasa na uhuru wa raia.

Kwa jumla, nchi ambazo hazicheleweshi uchaguzi katika tathmini iliyofanyika 2018 zilikuwa asilimia 11 juu zaidi kuliko zile ambazo zinachelewesha. Nchi ambazo hazina ucheleweshaji pia zilipata asilimia 24 juu zaidi katika mchakato wa uchaguzi na ushiriki wa vyama vingi vya siasa.

Hakuna nchi ambazo zilipata alama za juu zaidi kwa matokeo ya jumla, ikiwemo Botswana, Cabo Verde, Mauritius na Afrika Kusini, zimekuwa zikishuhudia ucheleweshaji.

Matokeo ya kustaajabisha

Lakini muangalio wa karibu unaonyesha matokeo ya kustaajabisha zaidi: Nchi ambazo zina alama za chini katika jadwali la viwango vya demokrasia, kama vile Burundi, Djibouti, Equatorial Guinea na Zimbabwe, hazijakumbwa na kuahirishwa uchaguzi.

Katika kipindi kilichoangazwa, nchi 10 zilizokuwa zinahisabiwa kuwa ni za “kidikteta” na kitengo cha Economist Intelligence zilichelewesha uchaguzi, lakini serikali 15 ambazo ziko katika kundi hilo hazikuchelewesha.

Kwa nchi ambazo zinania ya kuboresha utawala bora na kutengeneza mazingira ya kushirikisha mchakato wa demokrasia, kucheleweshwa kwa uchaguzi kunaweza kutumika kuimarisha ushiriki wa wapiga kura na kuwapa moyo wapiga kura bila ya uvunjifu wa amani au kuwalazimisha. Lakini serikali ambazo zinafanya uchaguzi ulio huru na wa haki hawana ulazima kutayarisha mipango hii.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG