Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 27, 2022 Local time: 02:36

Matokeo ya uchaguzi wa urais Nigeria kuanza kutangazwa Jumatatu


Maafisa wa uchaguzi wakitayarisha matokeo ya uchaguzi katika kituo cha kuhisabu kura Kano, kaskazini mwa Nigeria Feb. 24, 2019.

Baadhi ya vituo vya kupigia kura nchini Nigeria viliendelea kuwa wazi Jumapili huku kura zikianza kuhesabiwa katika uchaguzi wa urais unaoonenaka kuwa ni vigumu kubashiri nani anaelekea kushinda.

Mwandishi wa VOA mjini Abuja anaripoti kuwa Tume huru ya uchaguzi nchini Nigeria- IINEC inatarajiwa kuanza kutangaza matokeo ya uchaguzi Jumatatu.

Mpaka siku ya Jumatatu vyanzo vya habari vinaripoti kuwa idadi ya vifo katika ghasia zinazohusiana na uchaguzi imeongezeka na kufikia watu 39.

Mwandishi wetu anasema kuwa INEC ilisema itapanga tena uchaguzi katika baadhi ya sehemu kwenye majimbo ya Lagos, Rivers na Anambra ambako upigaji kura ulivurugika siku ya jumamosi. Hata hivyo haikufahamika mara moja ni wilaya zipi zilizoathiriwa.

Rais aliyeko madarakani Muhammadu Buhari na mpinzani wake mkuu, Atiku Abubakar wanatabiri ushindi wao katika kinyang'anyiro hicho.

Chama cha Peoples Democratic party cha Abubakar kilisema kimefanya vizuri katika maeneo kadhaa ikiwemo mji mkuu wa kibiashara wa Lagos. Abubakar alitoa taarifa akisema kwa matamshi yake “hivi punde jinamizi la miaka minne iliyopita litafikia mwisho ili kwa pamoja tuifanye Nigeria ifanye kazi tena.

Licha ya kupanga tena uchaguzi kwa baadhi ya majimbo, INEC ilisema iliridhishwa na upigaji kura, kwa mujibu wa shirika la habari la Ufaransa.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Washington, DC.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG