Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 15, 2024 Local time: 05:57

Guterres atahadharisha Janga la Covid-19 kuendelea mwaka 2022


Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres Alhamisi ametabiri kwamba janga la corona litakuwepo hata mwaka ujao akiongeza kwamba chanjo pekee hazitoshi kutokomeza  COVID-19.

Amesema kwamba chanjo zinapunguza idadi ya vifo pamoja na kulazwa hospitali, lakini maambukizi yangali yanaendelea kutokana na ukosefu wa usawa wa chanjo, kasi ndogo pamoja na kusita kupokea chanjo.

Guterres ameyasema hayo kwa wanahabari kwa njia ya mitandao baada yake kuwa amekutana na watu kadhaa ambao baadaye waligundulika wana virusi vya corona, akiwemo msemaji wake mkuu. Tangu Jumatano, Guterres amekuwa akifanyia kazi nyumbani kwake mjini New York ikiwa kama njia ya kuchukua tahathari.

Hii imekuwa mara ya pili ndani ya wiki moja kwa Umoja wa Mataifa kusema kwamba Guterres mwenye umri wa miaka 72 na ambaye amepokea chanjo kamili huenda amekutana na watu waliopata maambukizi na hivyo anafanyia kazi nyumbani kwake.

XS
SM
MD
LG