Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 04, 2023 Local time: 16:34

UN yaonya operesheni ya ukamataji inayoendelea Ethiopia


Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed

Umoja wa Mataifa umetoa tahadhari Jumanne wakati ukamataji mkubwa unaendelea nchini Ethiopia tangu nchi hiyo ilipotangaza hali ya dharura Novemba 2.

Shirika la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa limesema wengi waliokamatwa katika mji mkuu wa Ethiopia , Addis Ababa, pamoja na huko Gondar, BahirDar na maeneo mengine walikuwa watu wenye asili ya Tigray.”

Kwa mujibu wa taarifa takriban watu 1,000 wanaaminika kuwa wamekamatwa, huku wengine wakiripoti kuwa idadi ni kubwa zaidi,” msemaji Liz Throssell aliwaambia waandishi wa Habari mjini Geneva.

Ukamataji ulianza tangu serikali ya Waziri mkuu Abiy Ahmed ilipotangaza hali ya dharura , wiki mbili zilizopita na baadae wapiganaji wa TPLF, wakatishia kuandamana kuelekea mji mkuu.

Mawakili pia wamesema maelfu ya wa-Tigray wamekamatwa kikatili tangu tangazo lilipotolewa la kuchukua hatua hiyo, ambalo linaruhusu maafisa wa usalama kukamata watu bila kuwa na kibali kwa yeyote anayetuhumiwa kuunga mkono makundi ya kigaidi.

Miongoni mwa waliokamatwa tangu hali ya dharura ilipotangazwa ni baadhi ya wafanyakazi wa umoja wa mataifa.

Hata hivyo katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake Stephanie Dujarric amerejea wito wake wa kutaka kuachilia haraka kwa wafanyakazi wa UN.

Umoja wa Mataifa na kusema pande zote zinazohusika katika mzozo wa Ethiopia zimefanya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.

XS
SM
MD
LG