Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 06:40

Msaada wa dharura watolewa kwa Ethiopia


Watu walioachwa bila makao Ethiopia
Watu walioachwa bila makao Ethiopia

Umoja wa mataifa leo umesema umetoa fedha za dharura kusaidia kugawa msaada wa kibinadamu na kulinda raia wanaoathiriwa na mzozo wa Ethiopia.

Mkuu wa idara ya huduma za dharura ya Umoja wa mataifa Martin Griffiths amesema ameruhusu utoaji wa dola millioni 40 ambazo zitasaidia kuanzisha shughuli za dharura katika jimbo la Tigray na maeneo mengine ya kaskazini yanayokumbwa na mzozo huo, pia kama hatua za mapema kushughulikia suala la ukame kusini mwa nchi.

Griffiths amesema mamillioni ya watu wanaishi katika hali ya hatari huku mzozo wa kibinadamu ukizidi kuongezeka, akiongeza kuwa katika nchi nzima, mahitaji yanazidi kuongezeka.

Griffiths amesema dola millioni 25 zimetolewa na fuko la Umoja wa mataifa la kukabiliana na dharura, nazo dola millioni 15 ni kutoka fuko la misaada ya kibinadamu kwa ajili ya Ethiopia lenye makao yake makuu nchini humo.

Taarifa ya Umoja wa mataifa imesema huko Tigray, Amhara na Afar pesa hizo zitasaidia mashirika ya misaada yanayotowa ulinzi na huduma nyingine za kuokoa maisha ya wale wanaoathiriwa na mzozo.

Katika maeneo ya kusini ya Somali na Oromia yanayokubwa na ukame, pesa za ziada zitasaidia mashirika ya misaada kugawa maji ya kunywa, pamoja na kuzuia magonjwa yanayosababishwa na matumizi ya maji machafu kama vile kipindupindu, na kusaidia kuhifadhi mifugo,

XS
SM
MD
LG