Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 17, 2024 Local time: 16:15

DRC yafufua matumaini ya kucheza kombe la Dunia


Golikipa wa timu ya taifa ya Congo Léopards Ley Matampi akiukosa mpira huku mshambuliaji wa Uganda Patrick Kaddu akifunga bao wakati wa michuano ya kombe la mataifa ya Afrika CAN 2019 mjini Cairo, Misri 22 Juni 2019.
Golikipa wa timu ya taifa ya Congo Léopards Ley Matampi akiukosa mpira huku mshambuliaji wa Uganda Patrick Kaddu akifunga bao wakati wa michuano ya kombe la mataifa ya Afrika CAN 2019 mjini Cairo, Misri 22 Juni 2019.

Timu ya Taifa ya Congo Leopard imerejesha matumaini yake ya kufuzu kucheza kombe la dunia Qatar 2022 baada ya kupindua meza na kuifunga timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars bao 3-0 nyumbani kwao kwenye uwanja wa Mkapa Mjini Dar es Salaam Tanzania

Timu ya Taifa ya Congo Leopard imerejesha matumaini yake ya kufuzu kucheza kombe la dunia Qatar 2022 baada ya kupindua meza na kuifunga timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars bao 3-0 nyumbani kwao kwenye uwanja wa Mkapa Mjini Dar es Salaam Tanzania.

Taifa Stars waliingia na matumaini katika mechi hii baada ya kupata ushindi nje ya nchi dhidi ya Benin huku wakiongoza kundi J lakini matumaini yao yaliota mbawa baada ya DRC kupata bao la mapema katika mchezo huo kunako dakika ya 6 lililofungwa na Gael Kakuta.

Magoli mengine ya DRC yalifungwa na Fasika Idumba na Ben Malango.

Kwa matokeo hayo DRC sasa imejikita kileleni katika Kundi J kwa pointi nane, moja mbele ya Taifa Stars na Benin ambaye baadaye atacheza na Madagascar.

Na katika mechi nyingine za kufuzu timu ya taifa ya Uganda Cranes imetoka sare ya bao 1-1 na Harambee Stars ya Kenya wakati Ethiopia imetoka sare ya bao 1-1 na miamba Black Stars ya Ghana.

Uganda almanusura washindwe nyumbani hadi pale makosa ya kipa wa Kenya Brian Bwire kuwafanya kuambulia pointi moja katika dakika ya 90. Kipa huyo wa Kenya alichelewa kuchukua mpira alipokuwa akijaribu kupoteza muda huku Kenya wakiwa mbele kwa bao 1-0.

Hata hivyo, Fahad Bayo aliruka haraka na kuupiga mpira wavuni kabla ya kipa kuudaka kabisa kutoka chini.

Michael Olunga alikuwa ameipatia Kenya bao la kuongoza katika dakika ya 62 alipofunga kwa kichwa mpira wa adhabu uliopigwa na Amos Nondi.

Kwa matokeo hayo, Uganda wana pointi tisa, moja nyuma ya vinara wa kundi hilo Mali ambao watacheza na Rwanda baadaye Alhamisi.

XS
SM
MD
LG