Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 09:40

Wapiganaji wa Tigray washutumiwa kwa ubakaji huko Amhara

Wapiganaji wa Tigray (TPLF) wakisalimiana katika mji wa Hawzen, kaskazini mwa Ethiopia (AP Picha na Ben Curtis).
Wapiganaji wa Tigray (TPLF) wakisalimiana katika mji wa Hawzen, kaskazini mwa Ethiopia (AP Picha na Ben Curtis).

Wanawake kutoka mji unayokaliwa kimabavu katika mkoa wa Amhara nchini Ethiopia wanawashutumu wapiganaji wa Tigray kwa kuwabaka wakiwa wamewaelekezea bunduki na kuwaibia.

Wanawake kutoka mji unayokaliwa kimabavu katika mkoa wa Amhara nchini Ethiopia wanawashutumu wapiganaji wa Tigray kwa kuwabaka wakiwa wamewaelekezea bunduki na kuwaibia.

Ripoti mpya ya Amnesty International inaelezea mashambulizi ya kutisha yanayodaiwa kufanywa huko Nifas Mewcha, eneo lililopo kaskazini mwa Amhara, katikati ya mwezi wa Agosti.

Kupitia mahojiano na wanawake 16, kikundi cha haki za binadamu chenye makao yake mjini London kilielezea kwa kina mwenendo wa ubakaji wa magenge, wizi, unyanyasaji wa kimwili na matusi. Ripoti hiyo pia inasema wapiganaji wa chama cha Tigrayan People’s Liberation Front, au TPLF, walipora na kuharibu vituo vya matibabu katika mji huo. Baadhi ya manusura waliozungumza na kikundi cha utetezi walisimulia matumizi ya matusi ya kikabila, mashambulizi ya kikatili. Katika baadhi ya matukio, wanawake walisema walibakwa mbele ya watoto wao.

Amnesty imewataka makamanda wa TPLF kuchunguza tuhuma hizo na kuwaondoa wahusika wote kwenye jeshi hilo.

XS
SM
MD
LG