Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 15:53

Wafanyakazi 22 wa UN raia wa Ethiopia wakamatwa Addis Ababa


Umoja wa mataifa Jumanne umesema kwamba wafanyakazi wake 22 raia wa Ethiopia walishikiliwa na serekali kuu ya Ethiopia mjini Addis Ababa, kufuatia uvamizi ulioripotiwa kuwalenga Wa-Tigray.

Wafanyakazi sita wa Umoja wa Mataifa wameachiliwa.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa, Stephane Dujarric, amewaeleza wanahabari kwamba wafanyakazi 16 bado wanashikiliwa, na wanafanyakazi na serekali ya Ethiopia moja kwa moja kuhakikisha wanaachiliwa.

Amesema hakuna maelezo yaliyo tolewa juu ya sababu ya kushikiliwa kwa wafanyakakazi hao ambao wanafanyakazi katika idara mbalimbali.

Amesema baadhi yao wameshikiliwa toka siku kadhaa zilizopita.

Maafisa wa usalama wa Umoja wa Mataifa wamewatembelea wafanyakazi hao walio shikiliwa.

Septemba 30 serekali ya Ethiopia iliwafukuza wafanyakazi saba wa Umoja wa Mataifa wanaofanyakazi katika idara ya misaada ya kibinadamu, na kusema walikuwa wanaingilia masuala ya ndani ya Ethiopia.

XS
SM
MD
LG