Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 04, 2022 Local time: 20:54

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa linakutana kujadili mzozo wa Ethiopia


Mzozo unaoendelea Ethiopia unazidi kuchukua sura tofauti

Katika mikutano ya awali ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa iliyomalizika hakuna azimio la msingi ambalo limefikiwa kumaliza mapigano lakini Marekani imeshikilia mamilioni ya dola za msaada kwa Ethiopia na imetishia kuchukua hatua kali dhidi ya wale ambao wanachochea huu mzozo

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linakutana Jumatatu kujadili mzozo wa kaskazini mwa Ethiopia wakati ambapo wapiganaji wanadai kusonga mbele kuelekea mji mkuu wa Addis Ababa.

Katika kikao cha New York, nchini Marekani watajadili mzozo wa kibinadamu ambapo takriban watu milioni nane wanakabiliwa na kile ambacho Umoja wa Mataifa inakielezea hali mbaya sana ya kukumbwa na njaa kali.

Mfano wa kikao katika baraza la usalama la Umoja wa Mataifa
Mfano wa kikao katika baraza la usalama la Umoja wa Mataifa

Katika mikutano ya awali ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa iliyomalizika hakuna azimio la msingi ambalo limefikiwa kumaliza mapigano lakini Marekani imeshikilia mamilioni ya dola za msaada kwa Ethiopia na imetishia kuchukua hatua kali sana dhidi ya wale ambao wanachochea huu mzozo.

Pande zote mbili zimekataa mapendekezo ya kufanya mashauriano ya ana kwa ana ili kumaliza mzozo ambao umedumu kwa takriban mwaka mzima.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG