Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 18:41

Aina mpya ya virusi vya corona Omicron yaenea katika nchi nyingine.

Mchoro wa kueleza kuhusu aina mpya ya kirusi cha corona Omicron.
Mchoro wa kueleza kuhusu aina mpya ya kirusi cha corona Omicron.

Aina mpya ya virusi vya corona Omicron vilivyogunduliwa Afrika kusini kwa mara ya kwanza vimeenea  katika nchi nyingine na kusababisha shirika la afya duniani-WHO, kuonya juu ya hatari zinazokuja na kuziasa baadhi ya nchi kupanua wito wao kutoa chanjo ya ziada  Booster.

Waziri wa afya wa Afrika Kusini Joe Phaahla amesema hakuna haja ya kuwa na taharuki kufuatia aina hiyo mpya ya virusi vya Omicron, licha ya kuwepo na kesi nyingi. Japan imekuwa nchi ya karibuni kabisa kuweka masharti magumu ikiwazuiya wageni kuingia nchini kwake kuanzia Jumanne.

Uingereza, Umoja wa Ulaya, na Marekani ni miongoni mwa walioweka masharti ya usafiri mapema kwa Afrika kusini na nchi nyingine jirani. Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guterres alisema ana wasiwasi mkubwa kutengwa ka eneo la kusini mwa Afrika akiongeza kuwa watu wa Afrika hawawezi kulaumiwa kwa kiwango kidogo cha utoaji wa chanjo katika bara la Afrika. Siku moja baada ya kugunduliwa Amerika kaskazini,

Rais Joe Biden ameiita aina mpya ya kirusi cha Omicron ni sababu ya kutia wasiwasi , na sio sababu ya taharuki. Amesema hakuna haja ya kuweka masharti ya kufunga shughuli kwa sasa kama watu wamechomwa chanjo na wanavaa barakoa zao.

Kesi zimegunduliwa Canada na Marekani zimesababisha kuwekwa masharti ya safari katika nchi nane zilizoko kusini mwa Afrika. Msemaji wa ikulu ya Marekani Jen Psaki amesisitiza jumatatu masharti ya usafiri yaliyowekwa yanayoiathiri Afrika kusini na nchi nyingine saba za kusini mwa Afrika hayana nia ya kuadhibu lakini ni kwa ajili ya kulinda watu wa Marekani.

XS
SM
MD
LG