Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 30, 2022 Local time: 19:30

Chombo cha anga za juu SpaceX kurejea ardhini baada ya ziara ya majaribio


Wawili mstari wa mbele, kutoka kushoto, wanaanga Bob Behnken na Doug Hurley wakati wa mazungumzo na NASA wakiwa katika kituo cha anga za juu cha kimataifa Jumamosi Agosti 1, 2020.

Wanaanga wawili wa Marekani Doug Hurley na Bob Behnken wako katika safari ya mwisho na sehemu muhimu ya majaribio ya chombo cha kampuni binafsi cha SpaceX kurejea duniani, Jumapili.

Chombo cha anga za juu cha SpaceX.
Chombo cha anga za juu cha SpaceX.


Doug Hurley na Bob Behnken walishiriki katika sherehe ya kuwatakia safari njema Jumamosi katika kituo cha anga cha kimataifa, saa kadhaa kabla ya safari yao iliyokuwa imepangwa kufanyika na chombo cha SpaceX Dragon.

Licha ya kuwepo na kimbunga Isaias kilichokuwa kinasogelea Florida, NASA ilisema hali ya hewa inaonekana kuwa nzuri kwa chombo hicho kutua majini siku ya Jumapili mchana katika Ghuba ya Mexico karibu na mji wa Panama, Florida.

Itakuwa ni mara ya kwanza kwa chombo hiki kutia majini katika kipindi cha miaka 45. Mara ya mwisho kutua kwa chombo kama hicho ilikua ni safari ya pamoja ya anga za juu ni pale Marekani na Urusi ziliposhirikiana mwaka 1975 katika safari iliyojulikana kama Apollo-Soyuz.

Kurejea kwa wanaanga hawa kutakamilisha ziara yao ya miezi miwili inayomaliza kipindi cha muda mrefu wa kutofanyika safari za anga za juu kwa upande wa Marekani, ambayo ilikuwa inategemea roketi zinazo safirisha wanaaga wa Russia kwenda kituo cha anga za juu baada ya Marekani kusitisha kupeleka vyombo vyake vya anga za juu.

Safari ya Hurley na Behnken kutoka Kituo cha NASA cha Anga cha Kennedy, Mei 30, imekifanya chombo cha SpaceX kuwa cha kwanza cha kampuni binafsi kupeleka wanaadamu katika sayari za juu.

Baada ya ufanisi huo hivi sasa SpaceX inaelekea kuwa chombo cha kwanza kuwarejesha watu duniani.

“Sehemu ngumu zaidi ni kukirusha chombo hiki kwenda angani , lakini hatua muhimu zaidi ni kuturejesha nyumbani,” amesema Behnken.

Kutua kwa salama, amesema Behnken “kutakamilisha” uwezo wa Marekani kusafirisha wanaanga wake na kuwarudisha.”

Kamanda wa Kituo cha Anga Chris Cassidy, ataendelea kuwepo katika kituo cha kimataifa na Warusi wawili hadi Oktoba.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG