Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 16:20

Netanyahu avishutumu vyombo vya habari kwa kuchochea maandamano


Waandamanaji wakiwa nje ya makazi ya Benjamin Netanyahu wakishinikiza ajiuzulu.
Waandamanaji wakiwa nje ya makazi ya Benjamin Netanyahu wakishinikiza ajiuzulu.

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amelaani ghasia zilizotokea jana wakati wa mapambano kati ya waandamanaji wanaomtaka ajiuzulu na polisi akilaumu vyombo vya habari kwa upendeleo na kuchochea maandamano hayo kufanyika.

Akizungumza wakati wa mkutano wa baraza lake la mawaziri hii leo Netanyahu amesema vyombo vya Habari vinaripoti maandamano hayo muda mwingi Zaidi na kupotosha Habari za ghasia.

Waziri mkuu huyo amezungumza baada ya maadamano makubwa ambayo hayajawahi kutokea dhidi yake tangu 2011 kutokana na tuhuma za ulaji rushwa.

Wakati huohuo polisi mjini Jerusalem wamewakamata watu 12 na kuwaondoa kwa nguvu idadi kubwa ya watu wengine waliokuwa wameweka kambi katika njia karibu na makazi ya waziri mkuu baada ya maandamano ya usiku kumtaka kongozi huyo ajiuzulu.

Maelfu ya Waisraeli waliandamana Jumamosi usiku kumtaka Netanyahu kujiuzulu kutokana na tuhuma za ulaji rushwa na jinsi serikali yake inavyokabiliana na janga la corona.

Vyombo vya Habari vinakadiria kulikuwepo na karibu watu elfu 15 waliowasili hadi makazi ya waziri mkuu wakibeba mabango yanayomtaja kama “waziri mhalifu.”

Maandamano ya Jumamosi yanripoiwa kuwa makubwa zaidi kati ya maandamano yanayofanyika kila wiki nje ya makazi ya Netanahu.

Maandamano dhidi ya waziri mkuu huyo wa muda mrefu yanafanyika kote nchini kutokana na hali mbaya ya uchumi ilioathiriwa na janga la corona.

XS
SM
MD
LG