Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 26, 2022 Local time: 12:22

Israel : Gantz aeleza masikitiko makubwa juu ya kesi ya Netanyahu


Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, Kiongozi wa mrengo wa kati Benny Gantz

Kiongozi wa chama cha mrengo wa kati cha Bulu na nyeupe cha Israel Benny Gantz, anasema leo ni siku ya masikitiko makubwa kwa Israel.

Hii ni baada ya Wizara ya Sheria kutangaza kesi ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu itaanza kusikilizwa tarehe 17 march, wiki mbili baada ya uchaguzi mkuu.

Netanyahu ambaye ni Waziri Mkuu aliyebaki madarakani kwa muda mrefu anakuwa kiongozi wa kwanza wa nchi hiyo kufunguliwa mashtaka akiwa madarakani.

Netanyahu anatuhumiwa kwa ubadhirifu wa mali ya umma, kuchukua hongo na kukiuka kiapo chake. Hata hivyo Netanyahu amekanusha kuhusika na makosa yote hayo.

Katika tamko, Wizara ya Sheria imesema Jaji Rivka Friedman-Feldman atasoma mashtaka hayo mjini Jerusalem, wakati Netanyahu akiwa mahakamani.

Kesi hiyo ikiwepo uwezekano wa kukata rufaa kadhaa, inaweza kuchukua miaka mingi.

Chini ya sheria za Israel waziri yoyote wa serikali anaeshtakiwa kwa kosa la uhalifu lazima ajiuzulu. Lakini hii haimhusu Waziri Mkuu na hivyo kama chama chake cha likud kitapata ushindi wa kutosha kitaunda serikali.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG