Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 13:39

UN yaonya juu ya maafa ya Israeli kuchukuwa ardhi ya Wapalestina


Kamishna wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu Michelle Bachelet.
Kamishna wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu Michelle Bachelet.

Kamishna wa Umoja wa Mataifa (UN) wa Haki za Binadamu Michelle Bachelet ameonya Jumatatu hatma ya mpango wa Israeli kuchukuwa kwa mabavu eneo la Ukingo wa Magharibi una uwezekano wa kuleta “maafa” kwa Israel, Wapalestina na eneo hilo, na italeta madhara makubwa juu ya fursa ya suluhisho la kuwa na mataifa mawili.”

Katika taarifa yake, Bachelet amesema, “ Kujiingiza katika eneo hilo ni kinyume cha sheria,” na kuwa jaribio lolote la kulitawala eneo la wapalestina ambalo tayari linakaliwa kimabavu na Israeli kunaweza kuendeleza na kuongeza hali mbaya ya uvunjaji wa haki za binadamu ambayo imekuwa ni sehemu ya mgogoro kati ya pande hizo mbili kwa miongo kadhaa.

“Wasiwasi wangu mkubwa ni kuwa hata uchukuaji ardhi ndogo kabisa utapelekea kuongezeka kwa uvunjifu wa amani na vifo, wakati kuta zinajengwa, vikosi vya usalama vya Israeli vinapelekwa katika eneo na watu wa pande hizo mbili wanafanywa wakaribiane zaidi," amesema Kamishna huyo.

"Mfumo wa sheria katika tabaka mbili uliokuwepo katika eneo hilo utatekelezwa na utakuwa na athari mbaya kwa maisha ya Wapalestina ambao ama hawawezi kufikia kabisa mkondo wa sheria au nafasi yao ni finyu kufikia mkondo huo."

Serikali mpya ya mseto ya Israeli, iliyoapishwa kuchukuwa madaraka katikati ya mwezi Mei na kuongozwa na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, ina mpango wa kuchukuwa takriban asilimia 30 ya eneo la Ukingo wa Magharibi, ikiwemo maeneo yanayokaliwa kwa nguvu na Waisraeli na maeneo ambayo yana idadi kubwa ya Wapalestina. Mpango huo wa serikali hauna ridhaa kamili ya umma wa Waisraeli.

Maafisa walikuwa wameashiria kuwa hatua hiyo inaweza kuchukuliwa mapema Jumatano, lakini muda wa idhini ya ya mwisho bado haiko bayana.

Maafisa wa Palestina wameupinga mpango wa Israel na kuikosoa Marekani baada ya utawala wa Rais Donald Trump kuiunga mkono Israeli kuchukuwa ardhi katika mpango wa amani uliotolewa mwezi Januari.

Israeli ilikamata eneo la Ukingo wa Magharibi katika Vita-vya-Siku Sita mwaka 1967 na kuendelea kuikalia kwa mabavu tangu wakati huo. Wapalestina wanataka ardhi hiyo iwe in sehemu ya taifa la siku za usoni.

XS
SM
MD
LG