Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 04:28

Wanaharakati Zimbabwe wakimbilia mafichoni


Polisi wakifanya doria katika mitaa ya Zimbabwe kukabiliana na maandamano dhidi ya serikali kipindi hiki cha maambukizi ya COVID-19, Harare, Zimbabwe, Julai 31, 2020. REUTERS/Philimon Bulawayo
Polisi wakifanya doria katika mitaa ya Zimbabwe kukabiliana na maandamano dhidi ya serikali kipindi hiki cha maambukizi ya COVID-19, Harare, Zimbabwe, Julai 31, 2020. REUTERS/Philimon Bulawayo

Shughuli za biashara zimesitishwa katika miji mikubwa nchini Zimbabwe, polisi wakishika doria kuzuia maandamano ya kupinga serikali yaliyoitishwa na wanasiasa wa upinzani.

Maandamano hayo ni ya kulalamikia ongezeko la visa vya ufisadi serikalini pamoja na hali ngumu ya maisha.

Wakosoaji wa Rais Emmerson Mngangagwa wanasema kwamba serikali yake inatumia mbinu za kimabavu kuwanyamazisha wapinzani, ilivyokuwa wakati wa utawala wa hayati Robert Mugabe, aliyepiga marufuku maandamano, kuwateka nyara na kuwakamata wanasiasa wa upinzani.

Mnangagwa amesema kwamba wanaopanga maandamanao wanapanga kuipindua serikali yake.

Chama chake za ZANU-PF, kimemshutumu Balozi wa Marekani nchini Zimbawe kwa kufadhili maandamano hayo, kikimtaja kuwa jambazi.

Maduka, masoko na benki vimefungwa katikati mwa Harare, polisi na wanajeshi wakishika doria.

Hasira inaendelea kupanda nchini Zimbawe kutokana na mdororo wa maisha ambao sasa umefikia asilimia 7000, ukosefu wa sarafu za nje katika soko la ubadilishanaji wa fedha, ukosefu wa dawa hospitalini na migomo ya madaktari.

Darzeni ya wanaharakati wameenda mafichoni huku wakitafutwa na polisi kwa kuitisha maandamano hayo.

Msemaji wa chama kikuu cha upinzani – Movement for democratic change – MDC, Fadzayi Mahere na mwandishi wa riwaya Tsitsi Dangarembga wameandika kwenye mitandao yao ya kijamii kwamba wanazuiliwa na polisi kwa kuandamana.

Mahere amechapisha video inayoonyesha polisi wakimkaribia na kumwambia asiwarekodi, na kwa sasa hapatikani kwa simu.

Msemaji wa polisi Paul Nyathi, amesema kwamba hali ya usalama nchini Zimbabwe ni tulivu.

Watu kadhaa waliuawa katika msako uliofanywa na wanajeshi wa serikali kufuatia maandamano ya Januari 2019.

Wakosoaji wa rais Mnangagwa wanadai kwamba anatumia janga la virusi vya Corona kuzima harakati za wakosoaji wake.

Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG