Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 07, 2022 Local time: 13:36

Afrika Kusini yatangaza maambukizi 10,107 kwa siku moja


Mfanyakazi wa afya akimhudumia mgonjwa katika kituo cha muda kilichowekwa na Madaktari bila ya Mipaka (MSF) wakati wa mlipuko wa COVID-19 kwenye kitongoji cha Khayelitsha karibu na Cape Town, Afrika Kusini July 21, 2020. REUTERS/Mike Hutchings

Idadi ya watu waloambukizi na ugonjwa wa COVID-19 nchini Afrika Kusini imevuka 500,000 baada ya siku ya Jumamosi kurikodi maambukizo 10,107 kwa siku moja.

Waziri wa Afya Zwelini Mkhize alitangaza Jumamosi usiku idadi hiyo mpya ambayo ndio kubwa zaidi nchi humo kwa siku.

Vyanzo vya habari vimeeleza maambukizo hayo hivi sasa ni zaidi ya asilimia 50 ya maambukizo yote yaliyoripotiwa katika nchi 54 za Afrika.

Afrika Kusini sasa ina jumla ya watu 503,000 wenye kuuguwa ugonjwa wa COVID-19.

Takwimu zinaonyesha watu 8,153 wamekufa kutokana na COVID -19 nchini humo. Afrika Kusini ina idadi ya watu milioni 58.

Kwa mujibu wa ripoti za tafiti mbalimbali duniani taifa hilo hivi sasa linashika nafasi ya tano duniani kwa kuwa na idadi kubwa zaidi ya maambukizo.

Nchi ambazo zina idadi kubwa ya maambukizo duniani ni Marekani, Brazil, Russia na India.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG