Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 08, 2024 Local time: 15:22

Burkina Faso: Machafuko yanaendelea kufuatia madai ya mapinduzi ya kijeshi


Wafuasi wa kiongozi aliyetangaza utawala mpya wa kijeshi Burkina Faso Ibrahim Traore demonstrate wakipeperusha bendera ya Russia, mjini Ouagadougou.
Wafuasi wa kiongozi aliyetangaza utawala mpya wa kijeshi Burkina Faso Ibrahim Traore demonstrate wakipeperusha bendera ya Russia, mjini Ouagadougou.

Majeshi ya usalama yamefyatua gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji wenye hasira nje ya ubalozi wa Ufaransa katika mji mkuu wa Burkina Faso Jumapili.

Wakati huo huo ghasia zimeendelea kufukuta katika taifa la Afrika Magharibi ambalo limekumbwa na misukosuko kufuatia madai ya mapinduzi ya pili ya kijeshi mwaka 2022.

Ghasia za karibuni zilianza Ijumaa, wakati maafisa wa ngazi ya chini wa jeshi walipotangaza kuwa wamempindua kiongozi wa serikali ya kijeshi, na kuchochea wasiwasi mkubwa kati ya mataifa yenye nguvu duniani kufuatia machafuko ya karibuni yaliyolikumba eneo la Sahel linalopambana na uasi wa Kiislam unaoendelea kukua.

Jumamosi jioni, kiongozi wa kijeshi, Paul-Henri Sandaogo Damiba, alisema hana nia ya kuachia madaraka na kuwasihi maafisa hao “warejeshe fahamu zao.”

Kiongozi wa kijeshi wa Burkina Faso Paul-Henri Sandaogo Damiba Machi 2, 2022, akiwa mjini Ouagadougou.
Kiongozi wa kijeshi wa Burkina Faso Paul-Henri Sandaogo Damiba Machi 2, 2022, akiwa mjini Ouagadougou.

Maoni yake yamekuja muda mfupi baada ya maafisa wa jeshi kupuuzia mapinduzi hayo wakisema ni “mgogoro wa ndani” ya jeshi na kusema kuwa mazungumzo “yanaendelea” kurekebisha hali hiyo.

Hali ya Mji mkuu iliendelea kuwa ya mvutano usiku kucha, huku waandamanaji walikusanyika katika barabara kuu za mjini Ouagadougou huku helikopta zikiwa zinazunguka juu yao.

Katika tamko lililosomwa katika televisheni Jumapili, maafisa hao waliodai kufanya mapinduzi walisema walikuwa wameondoa amri ya kutotoka nje ambayo waliiweka na kuitisha mkutano wa wakuu wote wa wizara baadae siku hiyo.

Maafisa hao walimshutumu Damiba kwa kujificha katika kambi ya jeshi ya utawala wa zamani wa ukoloni wa Ufaransa ili kupanga “kujibu mashambulizi,” tuhuma ambazo yeye na Ufaransa wamezikanusha.

Siku ya Jumapili, darzeni za wafuasi wa kiongozi mpya wa mapinduzi aliyejitangaza, Ibrahim Traore, walikusanyika kwenye ubalozi wa Ufaransa katika mji mkuu.

Majeshi ya usalama yalifyatua gesi ya kutoa machozi kutoka ndani ya eneo hilo kuwatawanya waandamanaji baada ya kuwasha moto katika vizuizi nje na kutupa mawe katika jengo hilo, huku wengine wakijaribu kupanda ukuta wa uzio, kulingana na mwandishi wa shirika la habari la AFP aliyekuwepo katika eneo la tukio

Hakuna ripoti zozote zilizotolewa hapohapo za watu kujeruhiwa.

Madai ya mapinduzi ya Ijumaa yalipelekea wimbi la ukosoaji wa kimataifa, ikiwemo Marekani, Umoja wa Afrika, Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya kikanda ya ECOWAS.

Chanzo cha habari hii kinatokana na shirika la habari la AFP

XS
SM
MD
LG