Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 20, 2024 Local time: 04:22

Ufaransa kutafakari upya mkakati wake wa kijeshi Afrika


Rais Emmanuel Macro na mkuu wa jeshi la Ufaransa Thierry Burkhard
Rais Emmanuel Macro na mkuu wa jeshi la Ufaransa Thierry Burkhard

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema kwamba anataka "kutafakari upya mikakati yote ya jeshi la Ufaransa katika bara la Afrika" na amewataka mawaziri wake na wakuu wa jeshi kulifanyia kazi suala hilo.

Macron alitoa maoni hayo alipokuwa akiwahutubia wanajeshi wa Ufaransa kabla ya gwaride la Julai 14 la Siku ya Bastille mjini Paris.

Maafisa wa Ufaransa wanaelekea Niger kesho Ijumaa kuelezea upya mkakati wa nchi hiyo wa kupambana na wanamgambo wa Kiislamu katika eneo la Sahel, huku maelfu ya wanajeshi wakijitayarisha kuondoka Mali, na wasiwasi ukiongezeka juu ya tishio linaloongezeka kwa mataifa ya pwani ya Afrika Magharibi.

Mapinduzi nchini Mali, Chad na Burkina Faso yamedhoofisha mchango wa Ufaransa katika makoloni yake ya zamani, yamewatia moyo wanajihadi wanaodhibiti maeneo makubwa ya jangwa na misitu, na kufungua mlango kwa ushawishi mkubwa zaidi wa Russia.

Wasiwasi umeongezeka kwamba kuondoka kwa wanajeshi 2,400 wa Ufaransa kutoka Mali - kitovu cha vurugu katika eneo la Sahel na ngome za washirika wa al Qaeda na Islamic State - kunazidisha ghasia, kuyumbisha majirani na kuchochea uhamiaji.

XS
SM
MD
LG