Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Februari 25, 2024 Local time: 11:23

Utalii waongezeka Ufaransa, COVID -19 yaibuka tena.


Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akiwa katika mkutano wa NATO Madrid
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akiwa katika mkutano wa NATO Madrid

Wakati utalii unaongezeka tena nchini Ufaransa , janga la COVID nalo linaibuka. Maafisa wa Ufaransa wamependekeza kwa watu kuanza tena kuvaa barakoa lakini haitaweka masharti kwa sasa yatakayowashtua wageni au kuanzisha tena maandamano ya kupinga serikali.

Kwa wasafiri na watalii wa ufaransa , watu wengi wameonekana kukaribisha pendekezo hilo la serikali wakati wengine pia wana wasiwasi kwamba hatua za kujikinga zinaweza kuhitajika.

Maambukizo hayo ya COVID yamepelekea watu kulazwa tena kwa wingi hospitali nchini ufaransa kuanzia wiki mbili zilizopitaambapo takwimu zinaonesha kuwa wagonjwa 1,000 wanalazwa hospitali kwa siku .

Maambukizo pia yanaongezeka ulaya na Marekani lakini ufaransa ina idadi kubwa ya watu hospitalini kulingana na makadirio ya dunia . Msemaji wa ufaransa Olivia Gregoire amesema hakuna mipango ya kurejesha kanuni za kitaifa zinazoweka masharti ya kukusanyika ndani ya nyumba na shughuli nyinginezo.

XS
SM
MD
LG