Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Julai 23, 2024 Local time: 17:58

Blinken kuanza mkutano wa G-20


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken

Uvamizi wa Russia, nchini Ukraine utakuwa agenda ya juu wakati waaziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken atakapokutana na mawaziri wengine wa mambo ya nje kutoka kundi la mataifa 20 yenye uchumi mkubwa wiki hii huko Bali, Indonesia.

Kabla ya kikao cha kwanza waziri Blinken alikutana na mawaziri wa mambo ya nje wa mataifa ya Atlantic, waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa, Catherine Colonna, waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock, na waziri wa mdogo wa wa Uingereza, na mkurugenzi wa siasa Tim Barrow.

Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje, Ned Price amesema katika taarifa kwamba wanajadili juhudi za pamoja kuipatia Ukraine msaada mwingine wa kiusalama na kibinadamu na kuangalia njia za kushughulikia tatizo la kidunia la upungufu wa chakua ambalo limetokana na hatua ya makusudi ya Russia kuharibu kilimo cha Ukraine.

XS
SM
MD
LG