Kiwanda hicho ambacho kilijengwa na ufadhili wa kibinafsi kwenye eneo la hekta 1.5 huko Komsilga, katika kitongoji cha mji mkuu, kitahakikisha dawa zinazotumiwa na watu wengi zinapatikana, maafisa wamesema.
Kitaanza kutengeneza katika miezi michache ijayo dawa kama vile paracetamol na dawa ya kurejesha maji mwilini kwa ajili ya kutibu ugonjwa wa kuhara, mkurugenzi mkuu Armel Coefe amesema.
“Uwezo wetu wa uzalishaji kwa sasa unakidhi mahitaji ya ndani na utasuluhisha tatizo la upungufu mkubwa wa uzambazaji,” Coefe amesema.
Waziri mkuu Ouedraogo amesema kiwanda hicho ni cha “muhimu kwa sababu kitasaidia kuwapatishia raia dawa za bei nafuu.”