Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 29, 2024 Local time: 19:29

Milipuko miwili yaua wanajeshi 15 nchini Burkina Faso


Ramani ya Burkina Faso
Ramani ya Burkina Faso

Milipuko miwili iliua wanajeshi 15 wa Burkina Faso Jumanne, jeshi limesema, likiwa shambulio la hivi karibuni katika msusuru wa mashambulizi kama hayo wakati nchi hiyo ikipambana na uasi wa wanamgambo wa kiislamu.

Milipuko hiyo miwili kwa kutumia vilipuzi ilitokea kwenye barabara kutoka Bourzanga kuelekea Djibo katika eneo la kaskazini , ofisi kuu ya jeshi imesema.

Taarifa ya jeshi imesema “Hasara katika matukio hayo mawili ni wanajeshi 15 waliouawa na mmoja aliyejeruhiwa.”

Taarifa hiyo imeongeza kuwa “moja ya magari katika msafara, ambayo ilikuwa imebeba wanajeshi, ilikanyaga kilipuzi karibu na wilaya ya Namsiguia katika mkoa wa Bam.”

Kifaa cha pili kililipuliwa kwa mbali na kusababisha maafa mengi wakati wanajeshi wakililinda eneo hilo ili kuwahudumia waathirika, taarifa ya jeshi imesema.

Wanamgambo wa kiislamu wenye ngome katika nchi jirani ya Mali walianza kuendesha mashambulizi ya kuvuka mipaka dhidi ya Burkina Faso na Niger.

Nchini Burkina Faso, mashambulizi yanayofanywa na wanamgambo hao wa kiislamu wenye uhusiano na Al Qaeda na kundi la Islamic State yameua maelfu ya watu na kuwalizimisha wengine milioni 1.9 kuhama makazi yao.

XS
SM
MD
LG