Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 13:58

Takriban wanamgambo 30 wauwawa na jeshi Burkina Faso


Wanajeshi wa Burkina Faso wakishika doria kwenye picha ya maktaba
Wanajeshi wa Burkina Faso wakishika doria kwenye picha ya maktaba

Mwanajeshi mmoja ameuwawa pamoja na wanamgambo 28 kwenye operesheni mbili za kijeshi kaskazini na mashariki mwa Burkina Faso kulingana na ripoti ya Jumatatu kutoka kwa jeshi.

Taifa hilo la Sahel lisilo na bandari limekuwa likikabiliana na wanamgambo kwa miaka 7 ambapo zaidi ya watu 2,000 wamepoteza maisha huku wengine zaidi ya milioni 1.9 wakilazimika kuondoka mwakwao. Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, makabiliano yamechacha mashariki na kaskazini mwa nchi ambako wanajihadi wanashirikishwa na kundi la kigaidi la Al-Qaida au Islamic State.

Jumapili jeshi lilisema kwamba limeanza mashambulizi mapya baada ya ukandamizaji kutoka wa waasi kwenye mji wa kaskazini wa Sebba. Vituo viwili vya waasi viliharibiwa wakati wa mashambulizi hayo, ambapo watu 18 na mwanajeshi mmoja waliuwawa. Vikosi maalum vikisaidiwa na jeshi la wanahewa Jumapili pia, viliharibu kituo muhimu cha magaidi karibu na mji wa Soam ulioko mashariki mwa kituo hicho kilichoharibiwa kabisa wakati wanagambo 10 wakiuwawa.

Silaha , magari pamoja na vifaa vya mawasiliano vilipatikana wakati wa operesheni hiyo,huku jeshi likiomba wakazi kutoa taarifa kwa vikosi vya usalama kuhusiana na magaidi wanaojaribu kujipenyeza kwenye jamii. Wakati zaidi ya asilimia ya nchi ikiwa mikononi wa waasi, kundi la kijeshi lililochukua madaraka Junuari limetangaza vita dhidi ya waasi kuwa kipaumbele chake.

XS
SM
MD
LG