Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 22, 2025 Local time: 12:45

Compaore kurejea Burkina Faso


Aliyekuwa rais wa Burkina Faso Blaise Compaore kwenye picha ya 2011.
Aliyekuwa rais wa Burkina Faso Blaise Compaore kwenye picha ya 2011.

Vyanzo vya serikali ya Burkina Faso pamoja na watu wa karibu wa aliyekuwa rais wa taifa hilo Blaise Compaore, ambaye amekuwa uhamishoni tangu mwaka 2014 wamesema kwamba atarejea nyumbani wiki hii ili kukutana na wakuu wa jeshi.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, Compaore anatarajiwa nchini Alhamisi au Ijumaa ambapo atalakiwa na kiongozi wa taifa, chini ya mpango wa maridhiano ya kitaifa.

Mjumbe aliyetumwa na kiongozi wa kijeshi kundi linaloongoza taifa hilo Paul Henri Damiba alikutana na Compaore wiki iliyopita mjini Abidjan, wakati taarifa zikisema kwamba rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara pia alimpokea kiongozi huyo.

Wakati akiwa Burkina Faso, Compaore atakaa kwenye nyumba ya serikali ambako rais Roch Marc Kabore alikuwa ameshikiliwa tangu kuondolewa madarakani Januari.

XS
SM
MD
LG