Haikufahamika mara moja kilichokuwa kikiendelea na hakuna taarifa zozote kutoka kwa kiongozi mpya Kapteni Ibrahim Traore, ambaye aliwekwa na kundi lile lile la maafisa wa jeshi ambao walimsaidia Damiba kutwaa madaraka katika mapinduzi ya Januari 24.
Siku ya Ijumaa, Traore alionekana kwenye televisheni ya taifa, baada ya siku moja iliyokumbwa na milio ya risasi karibu na kambi ya jeshi, mlipuko karibu na ikulu ya rais na televisheni ya taifa ilizima matangazo.
Akiwa amezungukwa na wanajeshi, alitangaza serikali kuvunjwa na mipaka kufungwa. Haijulikani mahali alipo Damiba.
Utulivu ulirejea tena mjini Ouagadougou mapema Jumamosi lakini sauti ya risasi zilisikika majira ya mchana na kuonekana kwa msafara wa wanajeshi maalum kulisababisha maduka kufungwa na baadhi ya watu kukimbia kwa ajili ya usalama wao.