Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 07, 2021 Local time: 09:22

Brexit : Bunge la Uingereza kupiga kura ya makubaliano Ijumaa


Bunge la Uingereza linapiga kura Ijumaa, kupitisha sehemu ya makubaliano kwa taifa hilo kujiondoa kutoka Umoja wa Ulaya.

Kura ya leo itahusu tu makubaliano ya Uingereza kujiondoa, na sio tamko tofauti la kisiasa kuhusu mahusiano hali ya baadae kati ya nchi hiyo na Umoja wa Ulaya.

Waziri Mkuu Theresa May, anafanya jitihada za dakika za mwisho kuwashawishi wabunge kupitisha makubaliano hayo aliofikia na EU, lakini wataalam wanasema anakabiliwa na uwezekano wa kushindwa kwa mara nyingine.

Hapo awali siku ya leo ndio ilikuwa imepangwa Uingereza kujiondoa rasmi kwenye umoja huo.

Hatua ya Uingereza kujiondoa EU iilkumbwa na changamoto nyingi sana Jumatano, kuliko ilivyokuwa awali, baada ya bunge kukataa mapendekezo mbadala manane ya Theresa May.

EU ilikuwa imekubali kusogeza mbele tarehe ya Brexit hadi Mei 22, iwapo makubaliano ya kujiondoa yataidhinishwa na bunge la Uingereza wiki hii.

Kama hawataidhinisha makubaliano hayo, mchakato wa kujiondoa utarefushwa hadi Aprili 12, Uingereza itahitajika kutoa mapendekezo jinsi ya kuendelea na mchakato wake wa kujiondoa EU.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG