Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 28, 2022 Local time: 15:27

Kujitoa kwa Uingereza EU kutazingatia maslahi ya wananchi


Donald Tusk

Rais wa Baraza la Ulaya amesema maisha ya watu yanapewa kipaumbele katika maamuzi yoyote ya mazungumzo ya Uingereza kujiondoa Umoja wa Ulaya (EU).

Donald Tusk amesema Ijumaa wakati akiwa na Waziri Mkuu wa Maltese Joseph Muscat huko Malta, ambako Tusk ameeleza muongozo wa Uingereza kujitoa kutoka Umoja wa Ulaya.

Tusk amesema muongozo huo unakusudia kupunguza wasiwasi na matatizo ambayo yamesababishwa na Uingereza kujitoa, ambayo amesema utazigusa nchi za Ulaya.

“Tunahitaji kuwafikiria watu kwanza. Raia kutoka nchi zote za Ulaya wanaishi, kufanyakazi na kusoma Uingereza na muda wa kwamba Uingereza itabakia kuwa mwanachama, haki zao zitalindwa kikamilifu. Lakini inabidi tulimalize suala la kujitoa na hatma ya kujitoa kwao kwa kuhakikisha kuna makubaliano, utekelezaji na kutokuwepo ubaguzi,” amesema rais huyo.

Tusk amesema Uingereza lazima iheshimu majukumu yake yote ya kifedha na madeni yake iliochukua kama mwanachama wa Umoja wa Ulaya.

“Itakuwa tunawatendea haki watu wote, jumuiya, wanasayansi, wakulima na wengine, kwani sisi sote, mataifa yote 28 tumeahidi na tunajukumu la kulipa fedha hizi,” amesema.

Tusk aliuweka wazi muongozo huo mbele ya nchi 27 zinazoendelea na uwanachama wake, wakati akiwa na Waziri Mkuu Muscat, ambae anashikilia urais wa Umoja wa Ulaya hivi sasa katika mzunguko wa uongozi huo.

Rais wa Baraza la Ulaya amejaribu kuondoa wasiwasi uliopo kwamba kutakuwa na chuki katika mazungumzo ya Brexit, akiwahakikishia kuwa Umoja wa Ulaya hautaiadhibu Uingereza katika mazungumzo yao ya kujitoa kwa sababu kitendo chao cha kujitoa ni adhabu tosha.

XS
SM
MD
LG