Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 07, 2024 Local time: 10:59

Uingereza: Waziri wa Brexit ajiuzulu, May aendelea kulishawishi Bunge


Dominic Raab (kushoto)
Dominic Raab (kushoto)

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May tayari anakabiliwa na jukumu zito la kulishawishi bunge kupitisha mkataba unaoruhusu Uingereza kujitoa kutoka Umoja wa Ulaya ikiwa ni pigo kwake Alhamisi baada ya Waziri wa Brexit Dominic Raab kujiuzulu.

"Siwezi kwa nia nzuri tu kuunga mkono mambo yaliyo pendekezwa katika makubaliano yetu na Umoja wa Ulaya,” Raaba amesema wakati akitoa tamko likiainisha kupinga kwake mkataba huo ambao alishiriki katika mazungumzo yake.

Raab yeye hasa alikataa ibara muhimu katika mkataba huo ambayo inaweka ushuru wa pamoja ambao utaondosha haja ya kuwepo sheria kali za mpakani kati ya Irelanda Kaskazini ambayo ni sehemu ya Uingereza na mwanachama wa Umoja wa Ulaya, Ireland wakati Uingereza na Umoja wa Ulaya wakitafuta makubaliano mapya ya kibiashara.

Amesema bila ya kuwa na siku maalum ya tarehe ya mwisho kwa maandalizi hayo itaiacha Uingereza bila ya udhibiti wa kidemokrasia juu ya sheria zinazoongoza himaya yake, na itapelekea “kuegemea zaidi upande mmoja” katika mazungumzo ya biashara ya siku za usoni.

Sarafu ya Uingereza pound ilishuka thamani vibaya sana ikilinganishwa na dola ya Marekani baada ya Raab kujiuzulu.

Akiongea Alhamisi katika bunge, Kiongozi wa chama cha upinzani cha Labour Jeremy Corbyn ameeleza kuwa rasimu ya mkataba huo ni “uharibifu na kufeli kukubwa.”

Amesema kujiuzulu kwa Raab, “Ni moyo upi kitendo chake cha kujiuzulu kinampa mtu yoyote katika sehemu hii au nchi hii?”

May ametetea makubaliano hayo, akiwaambia wabunge itamaanisha kuwa Uingereza itajiondoa kutoka Umoja wa Ulaya “katika hali ya utulivu na utaratibu mzuri.

“Hatua hii inarejesha udhibiti wa mipaka yetu, sheria na fedha, inalinda ajira, usalama na hadhi ya Uingereza, na inatuwezesha kufikia malengo kwa njia nyingi kama wengi walivyosema wa kifupi jambo ambalo halikuwezekana kufikiwa huko nyuma,” amesema.

XS
SM
MD
LG