Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 04, 2023 Local time: 12:32

Waziri Mkuu May: Trump amekubali kuisaidia NATO kwa asilimia 100


Rais Donald Trump na Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May

Katika mkutano wake wa kwanza na kiongozi wa kigeni, Rais Donald Trump amesema Marekani na Uingereza “zinauhusiano maalum.”

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May amekubaliana na hilo, huku akitaja maslahi ya pamoja ya kiuchumi na maadili sawa kuwa ni mfano, lakini pia akasisitiza kuwa rais mpya ameahidi kuisaidia NATO kwa “asilimia 100.”

Trump amesababisha manung'uniko makubwa katika miji ya Ulaya kwa kauli zake kuhusu NATO kuwa imepitwa na wakati na kuwa wanachama wake wanatakiwa kulipa hisa zao kwa ajili ya ulinzi wao wenyewe.

Katika mkutano wa viongozi hao na waandishi wa habari, Trump amesema Uingereza ni nchi iliyoko moyoni wake kwa sababu mama yake anaasili ya Scotland.

“Leo hii Marekani inarejesha upya mafungamano yetu ya dhati na Uingereza- Kijeshi, kiuchumi, kiutamaduni na kisiasa. Tunauhusiano wa dhati,” amesema rais.

“Tunaahidi kuendeleza mahusiano haya muhimu. Kwa pamoja Marekani na Uingereza ni alama ya mafanikio na utawala wa sheria. Ndio maana Marekani inaheshimu uhuru wa wananchi wa Uingereza na haki yao ya kuamua wanachokitaka. Uingereza iliyo huru na yenye kujitawala ni heri kwa ulimwengu na mahusiano yetu siku zote yamekuwa imara.”

Trump amesema anaiunga mkono Uingereza kwa nguvu zote katika kura ya “Brexit” ilioitoa kutoka Umoja wa Ulaya. “Nafikiri Brexit itakuwa ni kitu kizuri kwa taifa lako,” alisema.

Amesema kuwa Uingereza itaweza kufikia “makubaliano huria ya kibiashara bila ya kusimamiwa na mtu yeyote katika kile mnacho kifanya.”

Msimamo wa Trump

Wakati waandishi wa habari katika chumba cha Ornate cha ikulu ya White House wanawauliza maswali viongozi hao, walidadisi kuhusu misimamo yenye utata ya Trump juu ya Mexico na Russia.

Alipoulizwa iwapo ataondosha vikwazo baada ya mazungumzo ya simu Jumamosi na Rais wa Russia Vladimir Putin, Trump amesema itakuwa ni mapema mno kuzungumzia mambo ya vikwazo.

Trump alisisitiza kuwa “anatarajia kuwa na mahusiano mazuri na nchi zote,” ikiwemo China.

Wakati anajibu swali hilo hilo, May amesema Uingereza inataka kuona vikwazo dhidi ya Russia vinaendelea mpaka pale mkataba wa Minsk utakapokuwa umetekelezwa kikamilifu—vipengere vinavyotaka kumalizika kwa mapigano kati ya waasi wanaofungamana na Russia na upande wa Ukraine.

NATO

May amesema moja kati ya maeneo muhimu ambayo nchi hizo mbili zinashirikiana ni vita dhidi ya kikundi cha Islamic State.

Pia amewastusha baadhi ya watu kwa kusema kuwa Trump amemwambia kuwa anakubali kuisaidia NATO, ambayo ni umoja wa kujihami wa nchi za Magharibi.

“Katika ushirikiano wa masuala ya ulinzi na usalama, tumeungana katika kuitambua NATO kama ni ngome ya ulinzi wetu wa pamoja na leo tumethibitisha msimamo wetu usiotetereka katika umoja huu. Bwana Rais, bila shaka umesema—na umethibitisha kwamba unaiunga mkono NATO kwa asilimia 100,”alisema May.

“Lakini bado tunajadili umuhimu wa NATO katika kuhakikisha kuwa inauwezo wa kukabiliana na ugaidi na vita vya mtandaoni kama vile itavyotakiwa kupigana vita vingine vya kawaida,” amesema.

“Pia nimekubaliana kuendelea kufanya juhudi ya kuwashawishi viongozi wenzangu katika Umoja wa Ulaya juu ya kutekeleza jukumu lao la kutumia asilimia 2 ya Kipato chao (GDP) katika ulinzi ili jukumu hilo lichangiwe sawa sawa na kila mmoja.

Links

XS
SM
MD
LG