Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:11

Wabunge wa Uingereza wapiga kura kuchukua udhibiti wa Brexit


Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May na mume wake Phillipe wakitoka kanisani baada ya ibada huko Sonning, Uingereza, Januari 6, 2019.
Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May na mume wake Phillipe wakitoka kanisani baada ya ibada huko Sonning, Uingereza, Januari 6, 2019.

Wabunge wa Uingereza wamepiga kura Jumatatu usiku kuchukua udhibiti wa hatua ya Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya -Brexit kutoka kwa Waziri mkuu Theresa May ili kujaribu kupata makubaliano yanayokubalika kwa wote Uingereza na Umoja wa Ulaya.

Kura hiyo ina maana kuanzia Jumatano wabunge watafikiri juu ya kutoa nafasi kwa mapendekezo kadhaa ambayo wanatumai yatakubalika kwa pande zote.

Kura katika bunge la Uingereza ilikuwa 329-302, ikiwa ni pamoja na mawaziri watatu wa serikali kujiuzulu nyadhifa zao ili tu waweze kupiga kura kuunga mkono hatua hiyo.

Serikali ya May, imeita hatua hiyo ya bunge kuwa ya hatari na isiyotabirika kwa mfano wa siku zijazo lakini ikatoa wito wa kutambua hali halisi.

Kura ya Jumatatu bungeni humo ina maana kuanzia Jumatano, wabunge watafikiri juu ya kutoa nafasi kwa mapendekezo kadhaa ambayo wanatumaini yatakubalika kwa pande zote ili kuwezesha Uingereza, kujitoa katika umoja wa Ulaya, kitu ambacho waziri mkuu May ameshindwa kukifanikisha na kuacha siku zijazo za serikali yake kuwa mashakani.

Imetayarishwa na Sunday Shomari.

XS
SM
MD
LG