Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 02:04

Brexit: May kuwasilisha ombi la kuongezewa muda.


Waziri mkuu wa Uingereza, Teresa May.
Waziri mkuu wa Uingereza, Teresa May.

Waziri mkuu wa Uingereza, Teresa May, anajitayarisha kuwasilisha ombi kwa Umoja wa ulaya la kucheleweshwa kwa angalau miezi kadhaa, kwa Uingereza kujiondoa kwa muungano huo ili kuuwezesha mchakato huo kuendelea kwa utaratibu.

Hii ni kufuatia kura mbili zilizopigwa na bunge la Uingereza wiki jana, ambapo mapendekezo ya May yalikataliwa huku spika wa bunge hilo, John Bercow, akiamuru kwamba wabunge hawangeendelea kupiga kura kwa hoja ambayo walikuwa wameikataa mara mbili hapo awali.

Karibu miaka mitatu imepita tangu Waingereza kupiga kura ya azma ya kujiondoa kwa muungano huo wa mataifa 28.

Msemaji wa May amesema huenda Waziri huyo mkuu akawasilisha barua ya kutaka kuongezewa muda siku ya Jumatano kwa rais wa baraza la Umoja wa Ulaya, Donald Tusk.

Wachambuzi wanasema ni vigumu kubashiri nini itakuwa hatima ya mvutano unaoendelea Uingereza na iwapo Uingereza itajitenga kama ilivyokusudiwa kwa kura ya mwaka 2016.

XS
SM
MD
LG